Mwizi aliyekutwa ndani ya gari la Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar, Farouk Karim.
Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar,
Farouk Karim, amesema kuwa siri kubwa ambayo mtu yeyote anaweza kuifanya
ili wezi watakapofika nyumbani kwake waibe lakini wapitiwe na usingizi
hapo hapo ni kumuamini na kumuomba Mungu ili awalinde wote ndani ya
familia.
Farouk ameyabainisha hayo leo Juni 2,
2020, wakati wa mazungumzo mubashara kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya
East Africa Radio, na ndipo aliposimulia mkasa wake baada ya mwizi
kuruka geti la nyumba yake huko Fuoni visiwani Zanzibar na kuiba nguo na
viatu lakini baadaye aliingia ndani ya gari na kupitiwa usingizi.
"Huyu mwizi kaingia usiku wa manane
karuka geti, na hatuna mlinzi pale nyumbani, kakusanya zile nguo
zilizokuwa zimeanikwa kaziweka kwenye mfuko, katika magari yaliyokuwepo
pale gari moja lilikuwa wazi akaingia, akapitia mlango wa abiria
akachukua power window, akaenda upande wa dereva kuchukua power window
ikamshinda ndiyo akalala hapo hapo" amesema Farouk Karim.
Akielezea siri ya mwizi kumuibia na kisha kupitiwa na usingizi Farouk amesema,"Tumempeleka
Polisi kama ambavyo huwa tuna msindikiza Bi harusi, na ile kulala
huenda kaiba sana hivyo karidhika, na dawa kubwa ya kumfanya mwizi alale
ni moja tu kumuomba Mungu akulinde wewe na nyumba yako, na watu kama
sisi ambao hatuna madhambi, Dua zinakubalika, kama unataka hiyo Dua
nitafute inbox".
Chanzo - EATV
No comments :
Post a Comment