*****************************
Na Magreth Mbinga
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh
Paul Makonda amesema wanaendelea na ujenzi wa ofisi za Walimu na
kuboresha huduma za afya kwa kutoa vifaa na wahudumu wa kutosha katika
hospitali ambazo zimejengwa kwa maelekezo ya Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Amezungumza hayo wakati wa kupokea vifaa tiba na ujenzi vilivyo tolewa na Mamlaka ya Bandari Tanzania Mgulani JKT.
Pia RC Makonda amesema anaishikuru
Mamlaka ya Bandari kwa kumvisha nguo wiki mbili zilizopita alitoa ahadi
ya mashine mbili za Utrasound na anazikabidhi Wilaya hiyo ili hospitali
ianze kufanya kazi kwa haraka.
Vilevile Naibu Mkurugenzi mkuu wa
Mamlaka ya Bandari Nchini TPA Eng Augustine Witonde wanaendelea kutoa
msaada ili kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Rais wametoa mashine
mbili za Utrasound kubwa na ndogo pia milango ya alminium 37na madirisha
27,milango ya magril 8 na madirisha 53 vyote hivyo vimetengenezwa na
Jeshi la Kujenga Taifa JKT.
Hatahivyo Eng Witonde amesema
vifaa vyote hivyo vinagharimu Milioni 60 na kuwataka wananchi waendelee
kutumia Bandari yao na rasilimali zake.
Sanjari na hayo Mkuu w Wilaya ya
Temeke Mh Felix Lyaviva amesema TPA hawapo mbali na Wilaya yake kwakuwa
mwaka jana walitoa mashuka na round Table kwaajili ya kujifungulia Leo
wameamua kukabidhi vifaa hivi naomba tuvipokee kwa mikono miwili
No comments:
Post a Comment