KWA mujibu wa vyombo vya habari
nchini Korea Kusini, Kim Jong-un, ameonekana hadharani kwa mara ya
kwanza baada ya siku 20 akiwa anakata utepe kwenye uzinduzi wa kiwanda
cha mbolea.
Shirika la habari la
taifa, KCNA limeeleza kuwa Kim aliambatana na maafisa kadhaa wa Korea
Kaskazini akiwemo dada yake Kim Yo Jong, jambo lililofanya watu
waliokuwepo kiwandani hapo kushangilia kwa furaha.
Haya hivyo, Shirika hilo la
habari halikutoa picha zozote wala kuelezea wapi alikuwa kiongozi huyo.
Naye Rais wa Marekani, Donald Trump, alipoulizwa kuhusu kuonekana kwa
kiongozi huyo alijibu “Siwezi kusema chochote kwa sasa.”
Taarifa kuhusu hali mbaya ya afya
ya Kim ilianza kusambaa baada ya kiongozi huyo kukosa kushiriki
maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa babu yake ambaye ni
mwanzilishi wa taifa hilo, Kim II Sung, mnamo Aprili 15, 2020.
Maadhimisho ya kumbukumbu hiyo
ni tukio kubwa sana katika matukio ya nchi hiyo, na Kim mara zote
hutembelea alipozikwa babu yake na hajawahi kukosa tukio hilo hapo
kabla.
No comments :
Post a Comment