Pages

Saturday, May 2, 2020

KIM JOG-UN AONEKANA HADHARANI




KWA mujibu wa vyombo vya habari nchini Korea Kusini, Kim Jong-un, ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza baada ya siku 20 akiwa anakata utepe kwenye uzinduzi wa kiwanda cha mbolea.

Shirika la habari la taifa, KCNA limeeleza kuwa Kim aliambatana na maafisa kadhaa wa Korea Kaskazini akiwemo dada yake Kim Yo Jong, jambo lililofanya watu waliokuwepo kiwandani hapo kushangilia kwa furaha.
Haya hivyo, Shirika hilo la habari halikutoa picha zozote wala kuelezea wapi alikuwa kiongozi huyo. Naye Rais wa Marekani, Donald Trump, alipoulizwa kuhusu kuonekana kwa kiongozi huyo alijibu “Siwezi kusema chochote kwa sasa.”


Taarifa kuhusu hali mbaya ya afya ya Kim ilianza kusambaa baada ya kiongozi huyo kukosa kushiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa babu yake ambaye ni mwanzilishi wa taifa hilo, Kim II Sung, mnamo Aprili 15, 2020.
Maadhimisho ya kumbukumbu hiyo ni tukio kubwa sana katika matukio ya nchi hiyo, na Kim mara zote hutembelea alipozikwa babu yake na hajawahi kukosa tukio hilo hapo kabla.

No comments:

Post a Comment