Thursday, February 27, 2020

SIO WANAWAKE TU HATA WANAUME WANAPIGWA WANANYANYASWA- RC MBEYA





Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akizungumza na vikundi vya wanawake wajisiriamali walijitokeza kuupokea msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akisalimiana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wanawake wajasiriamali wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akinywa juice iliyotengenezwa na wanawake wajasiriamali wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. William Paul Ntinika pamoja na wasanii Shetta, G Nako na wawakilishi wa Msafara wa kijinsia wa kutokomeza Ukatili wa kijinsia wakicheza wimbo maalum wa Kampeni ya Twende Pamoja.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. William Paul Ntinika akiwa katika picha ya pamoja na Msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia mara baada ya kuwasili mkoani hapo.
 Msanii Shetta na G Nako wakitumbuiza katika Stendi ya Kabwe mkoani Mbeya wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika soko la kabwe jijini Mbeya wakati Msafara wa kijinsia uliposimama mkoani humo kwa ajili ya kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia
havitokei kwa wanawake pekee bali hata wanaume wanapigwa na kunyanyaswa na wanawake.
Hayo yamesemwa kwa niaba yake leo mkoani humo na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. William Paul Ntinika alipokuwa akiupokea msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Mhe. Ntinika amesema kuwa jamii imekuwa iikiweka nguvu katika kuwatetea wanawake kwa kuwa wamekuwa wakitoa taarifa ya kufanyiwa vitendo vya ukatili kwa wanawake hivyo nguvu pia inahitajika ya kutoa elimu kwa wanaume ili waweze kutoa taarifa ya vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa Serikali inaendelea katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa dhidi ya wanawake na watoto kwa kuanzisha mipango na Sera mbalimbali zinazosaidia kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
“Sisi mkoa wa Mbeya tuko vizuri tunapambana na vitendo vya ukatili juzi tu tulipata taarifa kutoka kwa mtoto kuwa anafanyiwa vitendo vya ukatili na baba yake na tumeshamchukulia hatua za kisheria”alisema
Akizungumzia malengo ya msafara wa kijinsia Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha amesema msafara huo umelenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia katika familia na jamii kwa ujumla.
“Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tumekuja na msafara wa kijinsia ili tuweze kutoa elimu kwa wanajamii kuhusu kupambana na vitendo vya ukatili” alisema
Kwa upande wake Balozi wa Kampeni ya Twende Pamoja Nurdin Bilal ‘Shetta’ amesema suala la mapambano ya ukatili wa kijinsia ni suala la jamii yote katika mapambano hayo hivyo wameungana na Serikali katika kuhakikisha elimu inaifikia jamii ili kuondokana na vitendo hivyo.

No comments :

Post a Comment