…………………………………………………………………………………………………………….
Joctan Agustino,NJOMBE
Kufuatia ongezeko la wimbi la changamoto ya ajira nchini
serikali kupitia wizara ya kilimo kwa kushirikiana na wadau imeanzisha
kongamano la fursa za
kilimo,ufugaji na uvuvi litakalokuwa likikutanisha
vijana kutoka kanda tofauti ili kubadilishana ujuzi na namna bora ya
kukabiliana na changamoto zinazokwamisha sekta ya kilimo.
Takwimu za serikali za 2014 zinaonyesha zaidi ya asilimia 67
ya nguvu kazi ya taifa ni vijana hivyo serikali inakila sababu ya
kuhakikisha inahamasisha miundombinu ya sekta hiyo kwani imekuwa ikitoa
ajira kwa kiasi kikubwa tangu uhuru.
Akifungua kongamano la vijana zaidi ya 200 kutoka mikoa ya
Iringa , Njombe na Ruvuma lililofanyika mjini Njombe kwa lengo la
kujengea uwezo pamoja na kujadili changamoto zinazokwamisha sekta hiyo
naibu waziri wa kilimo Omary Mgumba anasema asilimia 35 ya watanzania
ambayo ni sawa na watu mil 16.1 ni vijana hivyo serikali imedhamilia
kuhamasisha vijana kushiriki katika kilimo ili kukabiliana na changamoto
ya ajira.
Awali mratibu wa kongamano la vijana katika kilimo taifa
Revelian Ngaiza na mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akiongea kwa
niaba ya mkuu wa mkoa wanasema kupitia jukwaa hili vijawana watabadili
mtazamo hasi walio nao katika sekta ya kilimo.Kwa upande wao vijana akiwemo Tulizo Ngata na Steven Mlimbila ambaye amepata mafanikio makubwa katika kilimo na kupata tuzo ya mkulima bora kanda ya nyanda za juu kusini kwa 2018 wanaseema kinachokwamisha vijana katika sekta hiyo ni mitaji na masharti magumu ya taasisi za kifedha.
Kongamano hilo la siku mbili ambalo limefanika kwa mara ya kwanza mkoani Njombe litafanyika pia katika kanda saba nchini likiongozwa na kauli mbiu isemayo “Vijana Kilimo ni Ajira”
No comments :
Post a Comment