Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe.
William Paul Ntinika akizungumza na vikundi vya wanawake wajisiriamali
walijitokeza kuupokea msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa
kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe.
William Paul Ntinika akisalimiana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu
ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha wakati msafara wa kijinsia
wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe.
William Paul Ntinika akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wanawake
wajasiriamali wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa
kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe.
William Paul Ntinika akinywa juice iliyotengenezwa na wanawake
wajasiriamali wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa
kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe.
William Paul Ntinika pamoja na wasanii Shetta, G Nako na wawakilishi wa
Msafara wa kijinsia wa kutokomeza Ukatili wa kijinsia wakicheza wimbo
maalum wa Kampeni ya Twende Pamoja.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe.
William Paul Ntinika akiwa katika picha ya pamoja na Msafara wa kijinsia
wa kutokomeza ukatili wa kijinsia mara baada ya kuwasili mkoani hapo.
Msanii Shetta na G Nako
wakitumbuiza katika Stendi ya Kabwe mkoani Mbeya wakati msafara wa
kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Baadhi ya wananchi
waliojitokeza katika soko la kabwe jijini Mbeya wakati Msafara wa
kijinsia uliposimama mkoani humo kwa ajili ya kutoa elimu juu ya ukatili
wa kijinsia.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Mhe. Albert Chalamila amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia
havitokei kwa wanawake pekee bali hata wanaume wanapigwa na kunyanyaswa na wanawake.
havitokei kwa wanawake pekee bali hata wanaume wanapigwa na kunyanyaswa na wanawake.
Hayo yamesemwa kwa
niaba yake leo mkoani humo na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. William Paul
Ntinika alipokuwa akiupokea msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa
kijinsia ulipowasili mkoani hapo.
Mhe. Ntinika amesema
kuwa jamii imekuwa iikiweka nguvu katika kuwatetea wanawake kwa kuwa
wamekuwa wakitoa taarifa ya kufanyiwa vitendo vya ukatili kwa wanawake
hivyo nguvu pia inahitajika ya kutoa elimu kwa wanaume ili waweze kutoa
taarifa ya vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa
Serikali inaendelea katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia
hasa dhidi ya wanawake na watoto kwa kuanzisha mipango na Sera
mbalimbali zinazosaidia kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo katika mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
“Sisi mkoa wa Mbeya
tuko vizuri tunapambana na vitendo vya ukatili juzi tu tulipata taarifa
kutoka kwa mtoto kuwa anafanyiwa vitendo vya ukatili na baba yake na
tumeshamchukulia hatua za kisheria”alisema
Akizungumzia malengo
ya msafara wa kijinsia Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo
ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha amesema msafara huo umelenga kutoa elimu
kwa jamii kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia katika familia na jamii
kwa ujumla.
“Kuelekea Maadhimisho
ya Siku ya Wanawake Duniani tumekuja na msafara wa kijinsia ili tuweze
kutoa elimu kwa wanajamii kuhusu kupambana na vitendo vya ukatili”
alisema
Kwa upande wake
Balozi wa Kampeni ya Twende Pamoja Nurdin Bilal ‘Shetta’ amesema suala
la mapambano ya ukatili wa kijinsia ni suala la jamii yote katika
mapambano hayo hivyo wameungana na Serikali katika kuhakikisha elimu
inaifikia jamii ili kuondokana na vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment