Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni
maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya
wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika
katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipeana mkono na Mjomba wa Marehemu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi)
aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni Maarufu, wakati akiwasili kwenye
makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, kuongoza mamia ya wakazi wa
Jiji la Dar es Salaam, katika mazishi ya Mfanyabiashara na Mwanazuoni
huyo, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni
maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya
wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika
katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Hussein Mwinyi, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua
Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi),
wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye
mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani jijini Dar es
Salaam, Novemba 29, 2019. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah
Ulega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
akiongea na wananchi baada ya mazishi ya aliyekua Mfanyabiashara na
Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), kwenye makaburi ya
Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
***********************************
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa ameongoza wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo
mengine kwenye mazishi ya Mfanyabiashara na Mwanazuoni Maarufu wa dini
ya Kiislam, Alhaj Aziz Massanga (Zingizi), yaliyofanyika katika makaburi
ya Msasani.
Alhaj Zingizi
amefariki dunia Jumatano, Novemba 27 jijini Johanesburg nchini Afrika
Kusini alikikwenda kwa ajili ya
kupatiwa matibabu. Marehemu Alhaj
Zingizi alikuwa akisumbuliza na ugonjwa wa saratani ya kibofu.
Akizungumza
baada ya mazishi hayo yaliyofanyika jana jioni (Ijumaa, Desemba 29,
2019), Waziri Mkuu aliwaasa wananchi kumuenzi marehemu Alhaj Zingizi kwa
kufanya mambo mema kama alivyokuwa akiyafanya enzi za uhai wake.
“Marehemu Zingizi alikua ni mtu mwenye kusaidia jamii kwa hali na mali.”
“Marehemu
ametenda mengi mema katika msikiti wake na jamii iliyomzunguka.
Alisaidia wenye mahitaji, hivyo na sisi hatuna njia nyingine ya kumuenzi
marehemu bali ni kutenda mema kwa jamii hususani kwa kuwajali watu
wenye shida ili wale waliokua wananufaika wasione pengo kubwa. ”
Waziri Mkuu
alisema kuwa Serikali ipo pamoja na viongozi wote wa dini na wala
wasisite kuijulisha pale wanapopatwa na jambo lolote ipo tayari
kushirikiana nao kwa namna moja au nyengine.
No comments :
Post a Comment