Pages

Saturday, November 30, 2019

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, katika mazishi ya Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi),

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mkono na Mjomba wa Marehemu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi) aliyekua  Mfanyabiashara na Mwanazuoni Maarufu,  wakati akiwasili kwenye makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, kuongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, katika mazishi ya Mfanyabiashara na Mwanazuoni huyo, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Mwinyi, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiongea na wananchi baada ya mazishi ya aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), kwenye makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
***********************************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine kwenye mazishi ya Mfanyabiashara na Mwanazuoni Maarufu wa dini ya Kiislam, Alhaj Aziz Massanga (Zingizi), yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani.
Alhaj Zingizi amefariki dunia Jumatano, Novemba 27 jijini Johanesburg nchini Afrika Kusini  alikikwenda kwa ajili ya
kupatiwa matibabu. Marehemu Alhaj Zingizi alikuwa akisumbuliza na ugonjwa wa saratani ya kibofu.
Akizungumza baada ya mazishi hayo yaliyofanyika jana jioni (Ijumaa, Desemba 29, 2019), Waziri Mkuu aliwaasa wananchi kumuenzi marehemu Alhaj Zingizi kwa kufanya mambo mema kama alivyokuwa akiyafanya enzi za uhai wake. “Marehemu Zingizi alikua ni mtu mwenye kusaidia jamii kwa hali na mali.”
“Marehemu ametenda mengi mema katika msikiti wake na jamii iliyomzunguka. Alisaidia wenye mahitaji, hivyo na sisi hatuna njia nyingine ya kumuenzi marehemu bali ni kutenda mema kwa jamii hususani kwa kuwajali watu wenye shida ili wale waliokua wananufaika wasione pengo kubwa. ”
Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ipo pamoja na viongozi wote wa dini na wala wasisite kuijulisha pale wanapopatwa na jambo lolote ipo tayari kushirikiana nao kwa namna moja au nyengine.

No comments:

Post a Comment