Saturday, June 29, 2019

FEDHA NA MADINI VYENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 3.125 VILIVYOTAISFISHA NA OFISI YA DPP VYAKABIDHIWA SERIKALINI



Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga (kushoto) akikabidhi sehemu ya fedha za kigeni kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James, wakati wa hafla ya kukabidhi fedha na madini vilivyotaifishwa na Ofisi ya DPP kutoka kwa watuhumiwa walioshindwa kwenye kesi zilizokuwa zikiwakabili kutokana na kukutwa na madini hayo. Hafla hiyo imefanyika ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam leo Juni 29, 2019.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Augustine Mahiga, (katikati) Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango (kushoto) na Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko, wakiwa wamekamata vitofali vya dhahabu ikiwa ni ishara ya serikali kupokea fedha na madini mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya shilingi bilioni 3.125 vilivyotaifishwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa  Mashtaka  (DPP), kutoka kwa watuhumiwa mbalimbali walioshindwa kwenye kesi zao wakishtakiwa kukutwa na fedha na madini hayo kinyume cha sharia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James, (kulia), akionesha kitofali cha dhahabu ikiwa ni sehemu ya shehena ya madini na fedha alivyopokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. Biswalo Mganga jijini Dar es Salaam Juni 29, 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James, (kulia), akipokea kisanduku chenye madini ya aina mbalimbali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka, Bw. Biswalo Mganga.
Mkurugenzi wa Mashtaka, Bw. Biswalo Mganga, (kushoto), akizungumza mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James (kulia), huku mawaziri kutoka kushoto na wizara zao kwenye mabano, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Fedha na Mipango), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Katiba na Sheria) na Mhe. Dotto Biteko, (Madini), wakati akikabidhi fedha na madini mbalimbali vilivyotaifishwa na serikali baada ya watuhumiwa waliokamatwa navyo kushindwa kwenye kesi zao
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James, (kushoto), akizungumza huku Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akisikiliza.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (katikati), akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (kushoto) na Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko, wakati wa hafla ya serikali kupokea fedha na madini vilivyotaifishwa na Ofisi ya DPP.
Dkt. Mahiga akizungumza
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (katikati) Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko, wakiongozana na maafisa wa juu wa serikali kuelekea ukumbi wa mikutano tayari kwa tukio hilo.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila, akizunhumza kwenye
tukio hilo.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
OFISI ya Mkurugenzi wa Mashtaka imeikabidhi serikali fedha taslim na madini mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya Zaidi ya
  shilingi bilioni 3.125.
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo yaliyofanyika ukumbi wa Serengeti wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Juni 29, 2019, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga alisema, fedha na madini hayo vilitaifishwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) katika vipindi tofauti kati ya mwaka 2017 na 2018.

"NPS imeendesha kesi mbalimbali zinzohusiana na utoroshaji au kukutwa na madini bila ya kuwa na kibali." Alisema Bw. Mganga muda mfupi kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James mbele ya  Waziri wa Sheria na Katiba, Mhe. Augustinen Mahiga, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko.
Aidha Bw. Mganga alisema hii ni mara ya pili Ofisi yake imekabidhi serikalini fedha na madini vilivyokamatwa  na kutaifishwa

No comments :

Post a Comment