Mkurugenzi
wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga (kushoto) akikabidhi sehemu ya fedha za
kigeni kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James,
wakati wa hafla ya kukabidhi fedha na madini vilivyotaifishwa na Ofisi
ya DPP kutoka kwa watuhumiwa walioshindwa kwenye kesi zilizokuwa
zikiwakabili kutokana na kukutwa na madini hayo. Hafla hiyo imefanyika
ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam leo Juni 29, 2019.
Waziri
wa Sheria na Katiba, Dkt. Augustine Mahiga, (katikati) Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philipo Mpango (kushoto) na Waziri wa Madini Mhe. Dotto
Biteko, wakiwa wamekamata vitofali vya dhahabu ikiwa ni ishara ya
serikali kupokea fedha na madini mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya
shilingi bilioni 3.125 vilivyotaifishwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashtaka (DPP), kutoka kwa watuhumiwa mbalimbali walioshindwa kwenye
kesi zao wakishtakiwa kukutwa na fedha na madini hayo kinyume cha
sharia.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James, (kulia), akionesha
kitofali cha dhahabu ikiwa ni sehemu ya shehena ya madini na fedha
alivyopokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. Biswalo Mganga
jijini Dar es Salaam Juni 29, 2019.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James, (kulia), akipokea
kisanduku chenye madini ya aina mbalimbali kutoka kwa Mkurugenzi wa
Mashtaka, Bw. Biswalo Mganga.
Mkurugenzi
wa Mashtaka, Bw. Biswalo Mganga, (kushoto), akizungumza mbele ya Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James (kulia), huku mawaziri
kutoka kushoto na wizara zao kwenye mabano, Mhe. Dkt. Philip Mpango
(Fedha na Mipango), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Katiba na Sheria) na
Mhe. Dotto Biteko, (Madini), wakati akikabidhi fedha na madini
mbalimbali vilivyotaifishwa na serikali baada ya watuhumiwa waliokamatwa
navyo kushindwa kwenye kesi zao
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James, (kushoto),
akizungumza huku Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango
akisikiliza.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (katikati), akiwa na
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (kushoto) na Waziri
wa Madini, Mhe. Dotto Biteko, wakati wa hafla ya serikali kupokea fedha
na madini vilivyotaifishwa na Ofisi ya DPP.
Dkt. Mahiga akizungumza
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila, akizunhumza kwenye
tukio hilo.
Aidha Bw. Mganga alisema hii ni mara ya pili Ofisi yake imekabidhi serikalini fedha na madini vilivyokamatwa na kutaifishwa
tukio hilo.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
OFISI
ya Mkurugenzi wa Mashtaka imeikabidhi serikali fedha taslim na
madini mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya Zaidi ya
shilingi bilioni 3.125.
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo yaliyofanyika ukumbi wa Serengeti wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Juni 29, 2019, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga alisema, fedha na madini hayo vilitaifishwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) katika vipindi tofauti kati ya mwaka 2017 na 2018.
"NPS imeendesha kesi mbalimbali zinzohusiana na utoroshaji au kukutwa na madini bila ya kuwa na kibali." Alisema Bw. Mganga muda mfupi kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James mbele ya Waziri wa Sheria na Katiba, Mhe. Augustinen Mahiga, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko.

No comments:
Post a Comment