Monday, April 29, 2019

UZINDUZI WA MAABARA YA KISASA TANZANIA YA KUIMARISHA UDHIBITI WA MIONZI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI


PMO_9195
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza, katika mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.
PMO_9201
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Meneja Muandamizi wa Kituo cha Kimataifa cha Sayansi na Teknolojia na Mshauri wa Masuala ya Kidiplomasia (ISTC), Dkt. Kamen Velichkov, baada ya kufungua mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.
PMO_9251
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe wakati alipozindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
PMO_9256
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati alipozindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
PMO_9289
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa kifaa cha kupimia mionzi na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi, Dkt Firm Banzi, baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
PMO_9340
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa kifaa cha kupimia vifaa vya kupimia mionzi na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi, Dkt Firm Banzi, baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
PMO_9357
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi cheti na pesa kwa kutambua uaminifu wao kwa Mtafiti wa Mionzi Daraja la Pili, Machibya Matulanya baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
PMO_9391
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 ………………………
Arusha,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo amezindua maabara ya kisasa ya kwanza katika ukanda wa
Afrika iliyogharimu zaidi ya sh,bilioni 8.38 ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania  iliyojengwa  na Serikali.

Waziri Majaliwa amesema maabara hii ni ya kipekee katika Bara la Afrika hivyo ni vyema wanafunzi,taasisi na Mashirika mbalimbali kutumia maabara hii ili kuwezesha sekta ya sayansi kukua zaidi kwani serikali inaendelea kujenga maabara za sayansi katika shule mbalimbali pamoja na kuajiri walimu wa masomo ya sayansi

Ameeleza kuwa sekta ya nyuklia ikitumiwa vizuri inaweza kuleta maendeleo katika sekta ya viwanda kwani serikali inaweka mkazo zaidi katika sekta ya viwanda kwa ajili ya kuinua uchumi ifikapo 2025

Amesema Serikali imejenga maabara hii ili kuhakikisha usalama wa wananchi dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi ya  kinyuklia “tunamshukuru Rais Magufuli kwa kuhakikisha maabara hii inajengwa Nchini kwani ni ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Bara la Afrika

Wakati huo huo, Majaliwa alifungua mkutano wa Wataalam wa Mionzi kutoka nchi za Jumuia ya maendeleo kusini mwa Africa(SADC) katika Kituo cha Mikutano cha Kimtaifa cha Arusha(AICC)

Umoja wa  Ulaya (EU) umefadhili bila ya masharti yoyote kwa serikali ya tanzania vifaa na mafunzo  kwa wataalamu watakaosimamia maabara hiyo kwa gharama ya sh, 6,669,782,984/40 na kwamba maabara hiyo itatoa huduma  katika nchi za Jumuia ya  Afrika ya Mashariki (EAC) na Nchi za SADC.

No comments :

Post a Comment