Tuesday, April 30, 2019

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MEI MOSI YAPAMBA MOTO SOKOINE MBEYA

????????????????????????????????????
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo kwa kamati ya maaandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya Wafanyakazi za Mei Mosi walipokutana nao kukagua maandalizi hayo katika Viwanja vya  Sokoine Jijini Mbeya Aprili 29, 2019.
????????????????????????????????????
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na kamati ya maaandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya Wafanyakazi za Mei Mosi walipokutana nao kukagua maandalizi hayo katika Viwanja vya  Sokoine Jijini Mbeya Aprili 29, 2019.
????????????????????????????????????
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akichangiua jambo wakati wa kikao hicho.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mjumbe Kamati ya Utendaji CWT Mwalimu Joyce Julius akichangia jambo katika kikao cha maandalizi ya sherehe za Mei Mosi kilichofanyika katika Viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya aprili 29, 2019.
????????????????????????????????????
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiangalia mazingira ya uwanja wa Sokoine utakaotumika kwa ajili ya Maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi kitaifa Jijini Mbeya alipokutana na kamati ya maandalizi ya sherehe hizo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na wajumbe wa kamati wakiwa katika ukaguzi wa maadalizi ya sherehe za Mei Mosi katika viwanja vya Sokoine Mkoani Mbeya.
????????????????????????????????????
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na kamati hiyo wakiangalia mtaro unaopitisha maji katika viwanja vya Sokoine ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufikia Kilele cha Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) Jijini Mbeya.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
……………………..
NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amekagua maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi na kusema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa.
Ametoa kauli hiyo Aprili 29, 2019 baada ya kupokea taarifa ya mbalimbali za Kamati ya Maandalizi walipokutana kujadili na kupanga mipango katika kuelekea kilele cha sherehe hizo zinazotarajiwa kuadhimishwa katika Viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya.
Waziri amesema Kamati ya Mkoa kwa kushirikiana na Ofizi yake imeendelea na maandalizi hayo na kuendelea kutoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kufika kwa wingi katika viwanja hivyo siku ya tarehe 1 Mei, 2019.
“Hadi sasa maandalzi yamefikia hatua nzuri na watu wanafanya kazi kwa umoja ili kuhakikisha shughuli hii inafana, wito wangu wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kuunga mkono wafanyakazi wa Tanzania katika siku yao hii muhimu.”Alisema waziri Mhagama.
Waziri aliwataka wanakamati hao wahakikishe wanasimamia vizuri wageni, pamoja na shughuli zote zitakazofanyika uwanjani hapo ili kuhakikisha wanaifikia siku hiyo kwa ushindi mkubwa.
Aidha Waziri aliongezea kuwa, uwepo wa maadhimisho hayo Jijini Mbeya wanachi wayatumie kama fursa ya kimaendeleo kwa kuwa mkoa utapokea wageni wengi hivyo waendelee kuwahudumia vyema.
Aidha kwa Upande wake rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya aliendelea kuhamasisha wananchi hususan wafanyakazi wote kujitokeza kwa wingi kuja kuiadhimisha siku hiyo.
“Ni wakati sahihi kwa wafanyakazi wote nchini kuitumia siku hii maalum katika kuiadhimisha na kuienzi ikiwa ni sherehe ya upekee sana hivyo mjitokeze kwa wingi pamoja na wananchi wote kwa ujumla.”Alisisitiza Nyamhokya.
Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi yatahadhimishwa Kitaifa katika Mkoa wa Mbeya ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, aidha maonesho hayo yatapambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo; Maandamano ya wafanyakazi na magari, Kwaya maalum, Nyimbo maalum kutoka kwa Vyama vya Wafanyakazi, wimbo maalum kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya, vikundi vya ngoma kutoka mikoa mbalimbali, Nyimbo maalum kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Kauli mbiu ya maonesha ya mwaka huu inasema; “Tanzania ya Uchumi wa Kati Inawezekana, Wakati wa Mishahara na Masilahi Bora kwa Wafanyakazi ni SASA”

No comments :

Post a Comment