Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akizungumza, katika mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya
Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akisalimiana na Meneja Muandamizi wa Kituo cha Kimataifa cha Sayansi na
Teknolojia na Mshauri wa Masuala ya Kidiplomasia (ISTC), Dkt. Kamen
Velichkov, baada ya kufungua mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa
Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe wakati alipozindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akiweka jiwe la msingi, wakati alipozindua Maabara ya Tume ya Nguvu za
Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akioneshwa kifaa cha kupimia mionzi na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi,
Dkt Firm Banzi, baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki
Tanzania Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akioneshwa kifaa cha kupimia vifaa vya kupimia mionzi na Mkurugenzi wa
Kinga ya Mionzi, Dkt Firm Banzi, baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya
Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akimkabidhi cheti na pesa kwa kutambua uaminifu wao kwa Mtafiti wa
Mionzi Daraja la Pili, Machibya Matulanya baada ya kuzindua Maabara ya
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa Maabara ya Tume
ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
………………………
Arusha,
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa leo amezindua maabara ya kisasa ya kwanza katika
ukanda wa
Afrika iliyogharimu zaidi ya sh,bilioni 8.38 ya Tume ya Nguvu
za Atomiki Tanzania iliyojengwa na Serikali.
Waziri
Majaliwa amesema maabara hii ni ya kipekee katika Bara la Afrika hivyo
ni vyema wanafunzi,taasisi na Mashirika mbalimbali kutumia maabara hii
ili kuwezesha sekta ya sayansi kukua zaidi kwani serikali inaendelea
kujenga maabara za sayansi katika shule mbalimbali pamoja na kuajiri
walimu wa masomo ya sayansi
Ameeleza
kuwa sekta ya nyuklia ikitumiwa vizuri inaweza kuleta maendeleo katika
sekta ya viwanda kwani serikali inaweka mkazo zaidi katika sekta ya
viwanda kwa ajili ya kuinua uchumi ifikapo 2025
Amesema
Serikali imejenga maabara hii ili kuhakikisha usalama wa wananchi dhidi
ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi ya kinyuklia
“tunamshukuru Rais Magufuli kwa kuhakikisha maabara hii inajengwa Nchini
kwani ni ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Bara la
Afrika
Wakati
huo huo, Majaliwa alifungua mkutano wa Wataalam wa Mionzi kutoka nchi
za Jumuia ya maendeleo kusini mwa Africa(SADC) katika Kituo cha Mikutano
cha Kimtaifa cha Arusha(AICC)
Umoja
wa Ulaya (EU) umefadhili bila ya masharti yoyote kwa serikali ya
tanzania vifaa na mafunzo kwa wataalamu watakaosimamia maabara hiyo kwa
gharama ya sh, 6,669,782,984/40 na kwamba maabara hiyo itatoa huduma
katika nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC) na Nchi za SADC.
No comments:
Post a Comment