Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na
Mipango kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Asanterabi Sang’enoi akizungumza
na wadau walioshiriki katika kikao kazi cha kujadili mfumo na nyenzo
kwa ajili ya udhibiti wa ukatili dhidi ya wanawake na watoto
utakaohusisha ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa, kutoa taarifa na
ufuatiliaji kilichofanyika katika ukumbi wa Umwema uliopo Mkoani
Morogoro Aprili 29, 2019.
Mchumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu
ambaye pia ni Mratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto Bi. Happiness
Mugyabusi akiwasilisha mada juu ya Mpango Kazi wa MTAKUWWA walipokutana
na wadau kutoka kwenye Wizara, Taasisi za Umma, Mashirika ya Kimataifa
na Asasi za Kiraia.
Dkt. Samwel Likindikoki Kutoka
MUHAS akiwasilisha mada kutoka kuhusu “INSPIRE Framework” kwa wadau
kutoka kwenye Wizara, Taasisi za Umma, Mashirika ya Kimataifa na Asasi
za Kiraia wakati wa kikao kazi hiko kilichofanyika Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wadau kutoka kwenye
wadau kutoka kwenye Wizara, Taasisi za Umma, Mashirika ya Kimataifa na
Asasi za Kiraia wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa mada wakati wa
kikao kazi hiko kilichofanyika katika ukumbi wa Umwema uliopo Mkoani
Morogoro Aprili 29, 2019.
Sehemu ya wadau wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao kazi hiko.
Maendeleo ya Jamii Mwandamizi
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw.
Mathias Haule akichangia mada wakati wa kikao hiko.
Mchumi kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu, Bw. Joel Mangi (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu mfumo wa
ujazwaji taarifa kwa wajumbe walioshiriki kikao kazi hiko kilichofanyika
Mkoani Morogoro.
Mchumi kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu, Bw. Joel Mangi (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu mfumo wa
ujazwaji taarifa kwa wajumbe walioshiriki kikao kazi hiko kilichofanyika
Mkoani Morogoro.
Mrakibu wa Magereza, SP. Amina
Kavirondo akichangia mada kuhusu masuala ya namna Jeshi hilo
linavyoshughulikia vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Wadau kutoka kwenye Wizara,
Taasisi za Umma, Mashirika ya Kimataifa na Asasi za Kiraia wakiwa kwenye
picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi hiko cha
kujadili
mfumo na nyenzo kwa ajili ya udhibiti wa ukatili dhidi ya wanawake na
watoto utakaohusisha ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa, kutoa taarifa
na ufuatiliaji kilichofanyika katika ukumbi wa Umwema uliopo Mkoani
Morogoro Aprili 29, 2019.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
…………………..
NA: MWANDISHI WETU
Mfumo wa Taifa wa takwimu za MTAKUWWA utasaidia kwa kiasi kikubwa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
Msaidizi wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Asanterabi
Sang’enoi wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau mbalimbali
kutoka kwenye Wizara, Taasisi za Umma, Mashirika ya Kimataifa na Asasi
za Kiraia kujadili mfumo na nyenzo kwa ajili ya udhibiti wa ukatili
dhidi ya wanawake na watoto utakaohusisha ukusanyaji na uchambuzi wa
taarifa, kutoa taarifa na ufuatiliaji kilichofanyika katika ukumbi wa
Umwema uliopo Mkoani Morogoro.
Alieleza kuwa lengo la mpango kazi
huo ni kuboresha mifumo itakayo saidia kuwa na taarifa na uwepo wa
takwimu sahihi ambazo zitasaidia kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na
watoto kwa asilimia 50 ifikapo 2022.
“Uwepo wa mfumo huo utawezesha
wadau kupata uelewa juu ya ukusanyaji wa taarifa na takwimu kwa kuandaa
taarifa ambazo zitasaidia kupima maendeleo ya Mpango Kazi wa Kudhibiti
Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto hapa nchini,” alisema Sang’enoi.
Aidha aliwataka wadau wa kikao
kazi hiko kushirikiana kwa pamoja ili waweze kuwa na mifumo ya taarifa
sahihi na takwimu rasmi za ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya
Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Bw. Mathias Haule alieleza kuwa Tanzania ni miongoni
mwa nchi zinazokabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto barani
Afrika kwa na inaongoza kwa kuwa na mifumo mingi ya ulinzi kwa wanawake
na watoto ikiwemo uanzishwaji wa madawati ya jinsia na watoto.
Naye, Bi. Lucy Tesha kutoka UN
Women alisema kuwa alisema kuwa kikao kazi hiko kitamwezesha kila mdau
kutambaua majukumu yake na kuweza kukusanya taarifa kwa kutumia mfumo
mmoja ambao utakuwa na data sawia ambazo zitakuwa hazijirudi kama
ilivyokuwa awali.
Pia, Mchumi kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu ambaye pia ni Mratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto Bi.
Happiness Mugyabusi alifafanua kuwa mpango kazi utasaidia kuwa na
takwimu za awali ambazo zitawezesha kutambua ndani ya miaka mitano ijayo
Taifa lilivyopiga hatua katika kutatua masuala haya ya ukatili dhidi ya
wanawake na watoto.
“Nchi yetu ina programu nyingi
zinazozingatia udhibiti wa ukatili dhidi ya wanawake na watoto lakini
wadau wameshindwa kuratibiwa vizuri kwa kukosa mfumo sahihi wa kukusanya
taarifa na hivyo kupelekea kuwaleta wadau kwa pamoja ili kuwa na
taarifa na takwimu za pamoja na uratibu mzuri wa wadau wote wa masuala
ya wanawake na watoto,” alisema Mugyabusi.
Katika kikao kazi hiko wadau
mbalimbali waliweza kushiriki ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu ambao ndio
waratibu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, MUHAS,
Mashirika ya Kimataifa (UN – Women), Asasi za Kiraia ( Child Watch, WFT,
TCRF, WILDAF, TGNP na TECDEN).
AWALI
Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza
Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA 2017/18 – 2021/22)
uliandaliwa kwa kuunganishwa mipango kazi tofauti iliyokuwa
inashughulikia ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
No comments:
Post a Comment