Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite,
Jummane Ngoma amefariki dunia leo Jumatano Januari 30, 2019 katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mtoto wa marehemu, Hassan Ngoma amesema, “Ni kweli Mzee amefariki leo jioni hii hapa Muhimbili,” amesema Ngoma
Hassan amesema kinachofanyika
kwa sasa ni kuuhifadhi mwili wa baba yake kisha baadaye watatoa taarifa
rasmi ikiwamo utaratibu wa msiba utakuwa wapi na mazishi yatafanyika
wapi baada ya kikao cha familia.
Aprili 6 mwaka jana, Rais John
Magufuli akizindua ukuta wa mgodi wa Tanzanite, Mirerani mkoani Manyara
alimzawadia Sh100 milioni kama shukrani kwa mchango wake kwa kugundua
madini hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wenginme wakimsikiliza
Mzee Jumanne Ngoma akitoa shukurani zake kwa kutambuliwa na serikali na
kupewa shilingi milioni 1000 na Rais kama ahsante yake wakati wa sherehe
za kuzindua rasmi ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani
wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara Aprili 6, 2018. Picha na Maktaba
No comments :
Post a Comment