Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)
Selemani Jafo akizungumza na wananchi alipokuwa akikagua utoaji wa
huduma katika zahanati ya Buza.
Wananchi
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani) alipofanya
ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)
Selemani Jafo akizungumza na wananchi alipokuwa akikagua utoaji wa
huduma katika zahanati ya Buza.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani).
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani) alipofanya
ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.
Wananchi
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani) alipofanya
ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.
..............................................................
Wananchi wa eneo
la Buza katika Manispaa ya Temeke Jijini
Dar es salaam wameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli
kwa ujenzi wa kituo cha afya Buza.
Shukrani hizo
wamezitoa leo wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni akiwa
safarini kuelekea wilayani Kibaha kukagua miradi ya maendeleo.
Alipofika
kituoni hapo, Waziri huyo alikutana na umati wa kinamama na watoto wakisubiri
kupata huduma katika Majengo yenye changamoto kubwa.
Akizungumza
na wananchi na wagonjwa waliokuwepo Kituoni hapo, Waziri Jafo amesema ameamua
kufanya ziara hiyo ili kujionea hali halisi ya wananchi hao wanavyopata huduma
ya afya.
“Serikali
inatambua changamoto zinazowakabili lakini nimeleta habari njema kwenu kuwa serikali
itakiboresha kituo hicho ili kuondoa kero zinazowakabili,”amesema.
Ameeleza
kuwa kituo hicho kitajengewa jengo la upasuaji,
wodi, maabara, jengo la wagonjwa
wa nje ikijumuisha vyumba vya madaktari
pamoja na jengo la X-Ray na mradi unaotarajiwa kugharimu zaidi ya sh.Bilioni
moja.
Kufuatia
hali hiyo, Wananchi hao wameishukuru serikali kwa kuendelea kutatua changamoto
zinazowakabili na kwamba uboreshaji huo utawawezesha waweze kupata huduma bora
za afya.

No comments :
Post a Comment