Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi (kushoto)
akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake katika utumishi wa umma kwa kufanya
kazi kwa miaka 41 Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu Mama Hadija Mradi katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo jijini
Dar Es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi Robert Mallya
Kaimu
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert
Mallya akimlisha keki Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu Mama Hadija Mradi wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika
leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar ES Salaam .
Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Afisa
Muuguzi Mwandamizi Mstaafu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mama Hadija Mradi (kulia) akikata keki wakati wa
hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Taasisi hiyo ilizopo jijini Dar Es Salaam.
Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi na kushoto
ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi Robert Mallya
Afisa
Muuguzi Mwandamizi Mstaafu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mama Hadija Mradi (kulia) akifuatilia yaliyokua
yakiendelea wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika Taasisi
hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa
wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa
hafla fupi ya kumuaga Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu Hadija Mradi (hayupo
pichani) iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo
jijini Dar Es Salaam.(PICHA NA JKCI)
NA
MWANDISHI MAALUM
WAFANYAKAZI
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kufanya kazi zao za kutoa
huduma kwa wagonjwa kwa uadilifu huku wakifuata sheria na kanuni za utumishi wa
Umma.
Rai
hiyo Imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi
wakati wa hafla fupi ya kumuaga Afisa Muuguzi Mwandamizi Mama Hadija Mradi
aliyestaafu utumishi wa Umma hivi karibuni.
Prof.
Janabi alisema wananchi hasa wagonjwa
wanategemea kupata huduma bora za matibabu ya moyo kutoka kwa wafanyakazi wa
Taasisi hiyo hivyo basi wajitahidi kufanya kazi zao kwa kufuata maadili
yaliyopo.
“Leo
hii tunamuaga Mama Mradi ambaye amefanya kazi ya Uuguzi kwa muda wa miaka 41, kama mama huyu
asingefuata maadili ya kazi yake siajabu
angefukuzwa kazi mapema lakini kutokana na uadilifu wake amefikia hatua ya
kustaafu salama hongera sana Mama kwa
kujitoa kwako kuwahudumia wagonjwa kwa miaka yote hiyo”, alisema Prof. Janabi.
Akizungumzia
jinsi anavyomfahamu Mama Mradi Kaimu
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi Robert
Mallya alisema mfanyakazi huyo alikuwa mfanyakazi bora ambaye alijituma katika
kazi zake bila ya kushinikizwa.
Mallya
alisema , “Ukimpangia majukumu ya kazi Mama Mradi atayatekeleza bila ya
kusimamiwa na kiongozi wake, kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi ndiyo
maana amefanya kazi muda mrefu hadi kufikia hatua ya kustaafu utumishi wa
umma ni muhimu kwa wauguzi tuliobaki
kazini tuige mfano wake”.
Kwa
upande wake Mama Mradi alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji, Viongozi pamoja na wafanyakazi wote wa Taasisi hiyo kwa
ushirikiano wao waliouonyesha kwa kipindi chote walichokuwa wanafanya kazi
pamoja na kuomba shirikiano huo uendelee.
Taasisi
hiyo ilimzawadi Mama Mradi zawadi zenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni saba
ambazo ni mabati 100 na mifuko 100 ya smenti hii ikiwa ni shukrani ya kutambua
mchango wake wa ufanyaji kazi alioutoa kwa utumishi wa Umma.
No comments :
Post a Comment