Tuesday, May 1, 2018

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA ULIVYOADHIMISHA SIKU YA MUUNGANO

Mhe. Baraka Luvanda (kulia), Balozi wa Tanzania nchini India akimpokea Mhe. Shri Vijay Goel, Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Taifa ya Tanzania iliyofanyika jijini New Delhi tarehe 26 Aprili 2018.
Mhe. Baraka Luvanda (kulia), Balozi wa Tanzania nchini India akiwa katika mazungumzo na Mhe. Shri Vijay Goel, Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India kabla ya kuanza rasmi kwa hafla ya kuadhimisha Siku ya Muungano wa Tanzania.

Balozi Luvanda akiwahutubia washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Muungano wa Tanzania

Balozi Luvanda akigongesheana glasi na Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India ikiwa ni ishara ya kuutakia mema Muungano wa Tanzania uweze kudumu milele.
Mhe. Shri Vijay Goel, Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India (katikati) akionesha jarida kuhusu miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuzinduliwa rasmi katika hafla hiyo.
Hafla ikiendelea
Mhe. Baraka Luvanda (kulia), Balozi wa Tanzania nchini India akimkabidhi zawadi ya kinyago Mhe. Shri Vijay Goel, Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India.

Picha ya pamoja.

No comments :

Post a Comment