Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akifungua mkutano wa wadau kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Chama cha Wenye Viwanda na Kilimo, (TCCIA) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kujadili masuala ya fidia kwa wafanyakazi kutoka mikoa ya Njombe na Iringa. Mkutano huo umefanyika mjini Iringa ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kilele cha Siku ya Wafanyakazi nchini ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Iringa.

Katinbu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mhe. Waziri akifafanua jambo wakati wa hotuba yake.
Mtendaji Mkuu wa ATE, Bw. Aggrey Mlimuka akizungumza.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba
Mshiriki akiuliza maswali ili kupata ufafanuzi

Mkurugenzi
Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (katikati), akiwa na Mkurugenzi wa Tiba
na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia) na Mkurugenzi wa
Uendeshaji, Bw. Anselim Peter, akifafanua baadhi ya hoja kutoka kwa
washiriki,
Baadhi ya washiriki wakipitia kipeperushi chenye taarifa za Mfuko
Mhe. Waziri akisalimiana na wafanyakazi wa WCF wakati akiwasili.
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, akizungumza
mwanzoni mwa mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko
huo, Bw. Anselim Peter.
Mhe. Waziri akizungumza jambo na viongozi wa WCF, na wadau wengine
Wanufaika wa fidia mahala pa kazi (mstari wa mbele), wakijumuika pamoja na washiriki wa mkutano huo.
Baadhi ya washiriki
Mshiriki akijisajili
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki
Picha ya pamoja
NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU,(KAZI, AJIRA NA VIJANA) ANTHONY MAVUNDE AFUNGA MKUTANO HUO
Katika
hotuba yake ya kuahirisha mkutano huo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira na Vijana, Mhe.
Anthony Mavunde, (pichani juu), amewashukuru washiriki kwa kujitokeza
kwa wingi kwenye mkutano huo, ambao lengo lake kuu ni kuendelea
kuelimishana kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi na kuhimiza waajiri
kujisajili na Mfuko. “Napenda kusisitiza kwamba, Mfuko huu uko kwa
ajili ya kuwasaidia sio tu wafanyakazi bali pia waajiri. “Nakumbuka
tulilazimika kuwapeleka mahakamni baadhi ya waajiri walioshindwa
kutekeleza takwa la kisheria la kujisajili na Mfuko, nia yetu haikuwa
kuwazalilisha waajiri bali ni jitihada za kuwakumbusha wajibu wenu.”:
Alisema, na kutolea mfano wa trafiki anapomuadhibu dereva kwa
kutokufunga mkanda, na tafsiri kwamba trafiki anajali sana usalama wako
kuliko wewe unavyojali usalama wako na hii si sawa, alisema. Aidha naibu
waziri ameutaka Mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wadau, ili waweze
kutekeleza sharia bila kisingizio chochote.
Naibu Waziri Mavunde akipongezwa na Bw. Mshomba baada ya kufunga mkutano huo. Kulia ni Mtendaji wa ATE, Bw. Aggrey Mlimuka.
Mhe. Naibu Waziri akiongozana na Bw. Mlimuka baada ya kufunga mkutano huo.
TANZANIA inaungana na mataifa
mengine kuadhimisha siku ya wafanyakaz Duniani (Mei Mosi), ambapo Serikali
imewakumbusha waajiri kote nchini, kuhakikisha haki za mfanyakazi zinalindwa.
Wito huo umetolewa mjini Iringa
leo Aprili 30, 2018 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi
, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama kwenye mkutano wa wadau kati ya
serikali, waajiri, pamoja na sekta binafsi kuhusu masuala ya fidia kwa
wafanyakazi.
sekta binafsi katika kukuza uchumi wa nchi na ndio maana inasisitiza mazingira
salama na endelevu ya mfanyaklazi mahala pa kazi ili shughuli za uwekezaji
ziendelee kwani nguvu kazi (wafanyakazi), watawajibika zaidi katika kufanya
kazi kwa vile wanatambua kuwa haki zao zinalindwa ikiwa ni pamoja na kulipwa
fidia stahiki endapo watadhurika wakati wakitekeleza wajibu wao wa kazi.
Mhe. Jenista alisema Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umekuja wakati muafaka kwani nchi inakwenda kwenye
uchumi wa viwanda bila shaka kutakuwepo na ongezeko la ajali na magonjwa
yanayotokana na uendeshaji wa shughuli katika viwanda, hivyo ni lazima kiwepo
chombo kitakachosimamia majukumu ya fidia ili kuwapa nafasi pana waajiri
kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.
“Tumekutana hapa leo ili
kuelimishana, wajibu wetu kama waajiri, tunapaswa kuhakikisha haki za
mfanyakazi zinalindwa na haki hizo ni pamoja na wewe mwajiri kujisajili na
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ili kumuhakikishia mfanyakazi kuwa endapo
ataumia, kuugua au kufariki wakati anatekeleza wajibu wake, basi atalipwa fidia
stahiki kulingana na madhara aliyoyapata na wategemezi wake watalipwa fidia
endapo mfanyakazi huyo atafariki na chombo pekee chenye jukumu la kufanya hivyo
ni WCF.” Alisema
Akieleza zaidi kuhusu faida za
mwajiri kujiunga na Mfuko huo, Mhe. Waziri alisema viwango vya juu vya malipo
ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya
kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa
mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema malipo
ya fidia kwa mfanyakazi aliyefariki ilikuwa ni shilingi 83,000/= ambazo walilipwa
wategemezi wake.
“Serikali ilikuja na sheria
mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali halisi, vilikuwa
vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata fidia hiyo kwa kadhia
kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa uchumi na kwa wakati
tulionao.” Alifafanua Mhe. Waziri.
Aidha Mhe. Waziri alisema,
Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa waajiri na taifa kwa
ujumla ambapo wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya kipato
kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo kutokana
na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa kushughulikia
masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao kwani
Serikali kupitia Mfuko itabeba mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi
atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.
“Pamoja na uchanga wake, Mfuko
huu ambao umeanzishwa mwaka 2015 umeonyesha mafanikio makubwa katika kipindi
kifupi kwani hadi sasa waajiri ambao wameshajisajili kwenye mfuko wetu ni
13,500 na wafanyakazi wao ambao wamepatwa na majanga wakiwa kazini wameshalipwa
fidia na Mfuko fedha zisizopungua shilingi bilioni 2.52 kufikia Februari 2018.”
Alibainisha.
Alisema Mfuko umekuja wakati
muafaka kwani nchi inakwenda kwenye uchumi wa viwanda bila shaka kutakuwepo na
ongezeko la ajali na magonjwa yanayotokana na uendeshaji wa shughuli katika
viuwanda vyetu hivyo ni lazima kiwepo chombo kitakachosimamia majukumu haya ya
fidia ili kuwapa nafasi pana waajiri kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.
“Rais wetu wa Jamhuri ya
uungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kila wakati tunapokutana kwenye
baraza la Wafanyabiashara Tanzania amekuwa akituagiza sisi wasaidizi wake, kama
kuna jambo lolote linajitokeza na sekta binafsi inafikiri kwamba jambo hili
bado halijaeleweka na haliko sawasawa ni wajibu wetu sisi mawaziri kuchukua
hatua haraka za kukutana na kujadiliana na wadau na kushauriana na wadau husika
ili kufikia muafaka na kuelewana ili kwenda pamoja na ndio maana leo tuko
hapa.” Alifafanua Mhe. Waziri Jenista Mhagama.
Wakitoa ushuhuda mbele ya
washiriki wa mkutano huo, Wafanyakazi waliopatwa na majanga ya kuumia au kufiwa
na wenza wao, wameipongeza Serikali kwa kuanzisha Mfuko huo kwani umekuwa ni
mkombozi kwa wafanyakazi.
Akitoam ushuhuda huo, mfanyakazi
wa Kampuni ya Frank Pile International Project Limited ya jijini Dar es Salaam,
Bw. Patrick Millinga, yeye alisema Mfuko umemlipa fidia ya zaidi ya shilingi
milioni 31.9 baada ya kupoteza jicho lake la kushoto kutokana na kugongwa na
kipande cha chuma wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi.
Mwingine aliyetoa ushuhuda wa
faida ya Mfuko kwa wafanyakazi, ni mama mjane, Bi. Petronila Mligo, ambaye yeye
alifiwa na mumewe katika ajali ya gari wakati akirejea kituo chake cha kazi
jijini Mwanza akitokea Dodoma.
“Mfuko umenilipa fidia ya
mkupuo kutokana na kifo cha mume wangu, lakini pia ninaendelea kulipwa pensheni
ya kila mwezi mimi na watoto wangu wawili, ambapo kila mtoto analipwa shilingi
175,000/= na mimi ninalipwa shilingi 375,000/=.” Alisema mama huyo mjane ambaye
ni mwalimu.
zamani, mfanyakazi anapotoka au kwenda kazini endapo atapatwa na tatizo njiani
sheria ya zamani haikumtambua, tofauti na sheria ya sasa ambapo inaeleza
mfanyaakzi akiumia au akifikwa na umauti wakati akitoka kazini au akielekea
kazini sheria ya sasa inataka afidiwe.
“Alisema Mfuko umeweka
utaratibu ili kuhakikisha mfumo wa usajili wa waajiri unakuwa wa haraka na
rahisi lakini pia kushughulikia masuala ya ulipaji fidia katika kipindi
kifupi.” Alisema.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID,
IRINGA

Mkutano huo
ambao ulikuwa ni sehemu ya shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi
inayofanyika kitaifa mkoani Iringa, umewaleta
pamoja wanachama
wa chama cha waajiri nchini, (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, (TPSF),
Taasisi ya Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo, (TCCIA), na Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, (WCF).
Serikali inatambua mchango waambao ulikuwa ni sehemu ya shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi

Akiwasilisha mada mbele ya
washiriki, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema Mfuko unaendeshwa
kwa msingi wa utatu ambapo katika bodi ya wadhamini ambayo ina uwakishi wa
serikali, wafanyakazi na uwakilishi wa waajiri kama ambavyo Shirika la Kazi
Duniani linavyotaka katika masuala haya ya fidia kwa wafanyakazi.
Alisema, katika mfumo wawashiriki, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema Mfuko unaendeshwa
kwa msingi wa utatu ambapo katika bodi ya wadhamini ambayo ina uwakishi wa
serikali, wafanyakazi na uwakilishi wa waajiri kama ambavyo Shirika la Kazi
Duniani linavyotaka katika masuala haya ya fidia kwa wafanyakazi.
zamani, mfanyakazi anapotoka au kwenda kazini endapo atapatwa na tatizo njiani
sheria ya zamani haikumtambua, tofauti na sheria ya sasa ambapo inaeleza
mfanyaakzi akiumia au akifikwa na umauti wakati akitoka kazini au akielekea
kazini sheria ya sasa inataka afidiwe.
“Alisema Mfuko umeweka
utaratibu ili kuhakikisha mfumo wa usajili wa waajiri unakuwa wa haraka na
rahisi lakini pia kushughulikia masuala ya ulipaji fidia katika kipindi
kifupi.” Alisema.
No comments :
Post a Comment