Tuesday, May 1, 2018

UDHAMINI WA PUMA NDANI YA IFA UTASAIDIA KUINUA VIPAJI VYA SOKA MKOANI IRINGA


Mkurugenzi wa kituo cha kuendeleza soka cha Iringa (IFA)  Ally Msigwa akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake akielezea mipango yake ya kuinua soka la vijana mkoani Iringa na Nje ya mkoa wa Iringa.
 Mkurugenzi wa kituo cha kuendeleza soka cha Iringa (IFA)  Ally Msigwa akionyesha jinsi ambavyo nembo ya puma iatapoa kwenye jezi za kituo hicho
Mkurugenzi wa kituo cha kuendeleza soka cha Iringa (IFA)  Ally Msigwa akiwa na kocha mkuu wa kituo hicho mwalimu Saleh molelikatika ofisi za IFA mkoani Iringa
 NA FREDY MGUNDA, IRINGA
KITUO cha kuendeleza soka cha Iringa (IFA) kimefanikiwa kuingia mkataba wa udhamini wa wa jezi na vifaa vya michezo kwa muda wa miaka miwili na kampuni ya mafuta ya Puma Energy.
Akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake, Mkurugenzi wa kituo cha kuendeleza soka cha Iringa (IFA)  Ally Msigwa, alisema kuwa kituo hicho kimepata udhamini wa vifaa vya michezo kutoka kampuni hiyo na udhamini huo utakijita kwenye safari zote za timu inapoelekea katika michezo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Iringa.
Msigwa alisema kuwa kituo hicho kimekuwa kimbilio la vijana wengi wenye vipaji na kimefanikiwa  kupata ufadhili wa kudumu kutoka kwa kampuni ya Alishati Investment ambayo itafadhili mahitaji mbalimbali katika kituo hicho.
 Alisema kuwa kituo hicho ambacho kimekuwa kikubwa kwa sasa kina mahitaji mengi ambayo yanahitajika katika kujikimu na kwa sasa kinatarajia kuwa na uwanja wake maeneo ya Ifunda kata ya Lumuli wilaya ya Iringa ambapo ujenzi wake uko katika mchakato kuanza baada ya kila kitu kukamilika.
Msigwa ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Yanga alisema kuwa katika ujenzi wa uwanja wanatarajia kujenga uwanja wa kisasa utakaochukua watu zidi 5000 hivyo kuwa moja ya viwanja bora kabisa kwa upande wa Nyanda za Juu Kusini.
Msigwa Aliongeza kuwa uongozi wa kituo hicho umeeamua kuunda bodi ya wakurugenzi ambao watasaidiana katika kufanikisha ndoto mbalimbali za kukuza soka la vijana nchini Tanzania ambapo Dk. Mshindo Msola ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa ufundi wa kituo hicho na kocha Salehe Molel kuwa kocha wa vijana chini ya miaka 15 hadi 17.
Aidha Msigwa alisema kuwa IFA imefanikiwa kuteua wajumbe wa bodi ambapo itaongozwa na Augustino Mahiga Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu ofisi ya Msajili Hazina Wizara ya Fedha Gerald Mwanilwa.
Wengine watakaounda wajumbe wa bodi ni Ezra Chomete mtanzania mwenye makazi Marekani, Abdul Mapembe ambaye ni Meneja TRA Ilala, Mhindisi Patrick Mbendule na Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa, Cyprian Kuyava.
Naye kocha mkuu wa kituo hicho mwalimu Saleh moleli alisema kuwa amepata sehemu sahihi ya kuujenga upya mpira wa mkoa wa Iringa kwa kuwa hapo awali alikuwa kocha anayefundisha timu za wakubwa tu.
“Kupata nafasi hii kwangu kama kocha mzoefu nimefarijika sana,nitakikisha naitumia vilivyo kwa kuahikisha mpira wa vijana unakuwa na kuzailisha kizazi cha soka hapa mkoani Iringa na duniani kwa ujumla” alisema Moleli
Moleli alisema kuwa watahakikisha vijana wote watakokuwa kwenye kituo hicho watapata elimu bila wasisi wowote ule.
“Wazazi wengi wamekuwa wakiwazuia watoto wao kukuza vipaji vyao kwa kuhofia kutoendelea na masomo yao lakini kwenye mpingo yetu kutakuwa na shule ambayo itawasaidia wanafunzi kusoma wakiwa hapo kituoni” alisema Moleli

No comments :

Post a Comment