Friday, February 2, 2018

WASHINDI 43 WA BAHATI NASIBU YA V.I.P CLUB INAYOENDESHWA NA BONITE BOTTLERS WAPATIKANA


Makasha yakiwa na tikei za bahati kutoka kwa Mawakala wa Bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha Vinywaji Baridi cha Bonite Bottlers cha mjini ,kinachoendesha Bahati nasibu kwa wateja wake wakubwa wajulikanao kama V.I.P Club .
Mwandishi wa Habari wa kituo cha radio cha Kili Fm ,Mwanahamisi Jingu akizungusha pipa lenye tiketi za bahati wakati wa droo ya kuwapata washindi iliyofanyika katika kiwanda cha vinywaji Baridi cha Bonite Bottlers Ltd cha mjini Moshi.
Mwandishi wa Habari Robert Minja akizungusha pipa lenye tiketi za bahati wakati wa droo ya kuwapata washindi iliyofanyika katika kiwanda cha vinywaji Baridi cha Bonite Bottlers Ltd cha mjini Moshi.
Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Bonite  Bottlers Ltd ya mjini Moshi Christopher Loiruk ,akitaja majina ya washindi katika Droo ya kupata washindi wa Bahati nasibu kwa Wateja wakubwa wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Zawadi za Pikipiki 25 zilizotolewa kwa washind wa Bahati Nasibu kwa wateja wakubwa wa bidhaa za Cocacola zinazozalishwa na Kampuni ya Bonite Bottlers ya Mjini Moshi.
Sanduku 100 na Sanduku 50 pia zilikuwa ni miongoni mwa zawadi ambazo washindi 43 walijinyakulia baada ya kushiriki bahati Nasibu hiyo.
Washiriki wa Bahati Nasibu kwa Wateja wakubwa wa Bidhaa jami ya Cocacola wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya baadhi yao kutangazwa washindi wa Droo iliyofanyika kiwandani hapo.
Washiriki hao walipata pia fursa ya kutembelea maene mbalimbali ya kiwanda hicho kujionea hatua mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa Jamii ya Cocacola.
Uzalishaji wa Cocacola ukiendelea katika kiwanda cha vinywaji baridi cha Bonite Bottlers cha mjini Moshi .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda a Kaskazini .
 
WASHINDI
wa bahati nasibu kwa wateja wakubwa wa Vinywaji baridi vya jamii ya CocaCola
wamepatikana baada ya Kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ya mkoani Kilimanjaro
kuchezesha droo ya kwanza ambapo jumla ya washindi 43 wamejinyakulia zawadi.
Miongoni
mwa zawadi kubwa ambazo washindi hao wamejinyakulia ni pamoja na Pikipiki 25
,sanduku 100 na sanduku 50 kwa washindi wata

No comments :

Post a Comment