Na Florah Raphael.
Waziri wa fedha na
mipango Dkt.Philip IsdorMpango amezindua rasmi ripoti ya uwasilishaji wa
matokeo ya makisio ya idadi ya watu leo jijini Dar es salaam ambapo
imeonekana kuwa Tanzania imekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu na
kubainika kuwa ifikapo mwaka 2021 idadi ya watu inakadiliwa kufikia
milioni 77.5
Akiongea katika
uzinduzi huo waziri Mpango amesema kuwa takwimu sahihi na kwa wakati
sahihi zinasaidia kuboresha maisha wa watu na katika kupanga maendeleo
ya muda mfupi, kati na muda mrefu ndani ya Taifa na kuongeza kuwa pia ni
muhimu katika kupanga bajeti ya serikali kwani inarahisisha serikali
kujua idadi ya nguvu Kazi waliyonayo.
Pia amesema kuwa
takwimj sahihi zinasaidia kujua huduma zinazohitajika na maeneo
yanayohitaji huduma hizo na kusisitiza kuwa wingi wa watu siyo tatizo
kwa nchi bali wingi wa ongezeko la watu unapozidi ongezeko la uchumi kwa
nchi ndio huweza kutokea changamoto.
Pia waziri Mpango
amesema kuwa kwa mjibu wa sensa ya mwaka 2012 kiwango cha utegemezi ni
92% ikilinganishwa na 42% kwa nchi zilizoendelea, hivyo Tanzania
kumekuwa na idadi kubwa ya watu waliotegemezi ambapo watu wenye umri
kati ya 15-64 wanategemewa na watu 98 kati ya 100 wenye umri chini ya
miaka 15 na wenye umri zaidi ya miaka 65.
Kutokana na
changamoto hiyo ya idadi kubwa ya watu tegemezi waziri Mipango amesema
kuwa serikali imechukua hatua za kukabiliana na changamoto hiyo kwa
kuamua kujikita na kuelekeza nguvu kubwa katika kuboresha elimu, kuweka
juhudi katika kuelekea uchumi wa Viwanda ambao utapelekea kutoa ajira
nyingi hasa kwa vijana, kutoa haki sawa kwa mwanamke na mwanaume
kumiliki Mali ikiwemo ardhi sambamba na kutoa elimu kuhusu matumizi ya
mpango wa uzazi.
Aidha waziri Mpango
ametoa onyo kwa mashirika yoyote ya Tanzania na nje ya Tanzania kutoa au
kuchapisha idadi ya watu wa Tanzania bila kushirikisha ofisi ya Taifa
ya takwimu na kusema kuwa wakifanya hivyo ni kosa kisheria kwa mjibu wa
shetia namba 9 ya mwaka 2015 na kuwaomba wadau wote wa takwimu kufuata
utaratibu wa matumizi ya takwimu rasmi za nchi popote walipo ili kuleta
maslahi kwa Taifa.
Aidha Mkurugenzi wa
ofisi ya takwimu Dkt.Albina Chuwa amesema kuwa idadi ya watu kuendela
kuongezeka ni jambo zuri kwani katika nchi inayohitaji maendeleo lazima
kuwepo na nguvu Kazi hasa vijana na kuongeza kuwa kwa sasa miaka ya
kuishi inakadiliwa kuwa 65 kwa sasa ukilinganisha na miaka iliyopita
ambapo miaka ya kuishi ilikuwa 37.
Pia Dkt.Chuwa amesema
kuwa kwa mjibu wa takwimu za umoja wa mataifa za mwaka 2017, dunia
ikadiliwa kuwa na watu wapatao bilioni 7.53, Afrika bilioni 1.25 nchi
zikizo kusini mwa jangwa la sahara bilioni 1.02 na kwa makadilio ya
sensa ya mwaka 2012 na kwa kuzingatia viwango vya uzazi na vifo kwa
takwimu za mwaka 2016, Tanzania inakadiliwa kuwa na idadi ya watu
wapatao milioni 54.2 ambapo Tanzania bara ni milioni 52.6 na Zanzibar
milioni 1.6 kwa mwaka 2018 hivyo idadi hiyo inakadiliwa kufikia watu
milioni 59.4 ifikapo mwaka 2021 na kufikia mwaka 2030 idadi ya watu
itafikia milioni 77.5.
Aidha mwakilishi wa
umoja wa mataifa UNFPA Jackiline Moha amesema kuwa si Tanzania tu yenye
kasi ya ongezeko la watu hali iko hivyo hata kwa nchi nyingine duniani
kote na kuongeza kuwa kwa Tanzania 44% ya watu ni vijana wenye umri
chini ya miaka 15 hivyo wakiangaliwa toka Kipindi cha ukuaji wao
watakuwa na mchango mkubwa kwa taifa hasa kwa vijana wa kike hivyo
serikali inatakiwa kufanya uwekezaji sahihi na kwa wakati sahihi kwa
vijana kwa kuwapatia elimu na afya bora.
No comments :
Post a Comment