Pages

Wednesday, February 28, 2018

TANZANIA YAKADILIWA KUWA NA WATU MILIONI 77.5 IFIKAPO MWAKA 2030

Mipango
Na Florah Raphael.
Waziri wa fedha na mipango Dkt.Philip IsdorMpango amezindua rasmi ripoti ya uwasilishaji wa matokeo ya makisio ya idadi ya watu leo jijini Dar es salaam ambapo imeonekana kuwa Tanzania imekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu na kubainika kuwa ifikapo mwaka 2021 idadi ya watu inakadiliwa kufikia milioni 77.5
Akiongea katika uzinduzi huo waziri Mpango amesema kuwa takwimu sahihi na kwa wakati sahihi zinasaidia kuboresha maisha wa watu na katika kupanga maendeleo ya muda mfupi, kati na muda mrefu ndani ya Taifa na kuongeza kuwa pia ni muhimu katika kupanga bajeti ya serikali kwani inarahisisha serikali kujua idadi ya nguvu Kazi waliyonayo.
Pia amesema kuwa takwimj sahihi zinasaidia kujua huduma zinazohitajika na maeneo yanayohitaji huduma hizo na kusisitiza kuwa wingi wa watu siyo tatizo kwa nchi bali wingi wa ongezeko la watu unapozidi ongezeko la uchumi kwa nchi ndio huweza kutokea changamoto.
Pia  waziri Mpango amesema kuwa kwa mjibu wa sensa ya mwaka 2012 kiwango cha utegemezi ni 92% ikilinganishwa na 42% kwa nchi zilizoendelea, hivyo Tanzania kumekuwa na idadi kubwa ya watu waliotegemezi ambapo watu wenye umri kati ya 15-64 wanategemewa na watu 98 kati ya 100 wenye umri chini ya miaka 15 na wenye umri zaidi ya miaka 65.
Kutokana na changamoto hiyo ya idadi kubwa ya watu tegemezi waziri Mipango amesema kuwa serikali imechukua hatua za kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuamua kujikita na kuelekeza nguvu kubwa katika kuboresha elimu, kuweka juhudi katika kuelekea uchumi wa Viwanda ambao utapelekea kutoa ajira nyingi hasa kwa vijana, kutoa haki sawa kwa mwanamke na mwanaume kumiliki Mali ikiwemo ardhi sambamba na kutoa elimu kuhusu matumizi ya mpango wa uzazi.
Aidha waziri Mpango ametoa onyo kwa mashirika yoyote ya Tanzania na nje ya Tanzania kutoa au kuchapisha idadi ya watu wa Tanzania bila kushirikisha ofisi ya Taifa ya takwimu na kusema kuwa wakifanya hivyo ni kosa kisheria kwa mjibu wa shetia namba 9 ya mwaka 2015 na kuwaomba wadau wote wa takwimu kufuata utaratibu wa matumizi ya takwimu rasmi za nchi popote walipo ili kuleta maslahi kwa Taifa.
Aidha Mkurugenzi wa ofisi ya takwimu Dkt.Albina Chuwa amesema kuwa idadi ya watu kuendela kuongezeka ni jambo zuri kwani katika nchi inayohitaji maendeleo lazima kuwepo na nguvu Kazi hasa vijana na kuongeza kuwa kwa sasa miaka ya kuishi inakadiliwa kuwa 65 kwa sasa ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo miaka ya kuishi ilikuwa 37.
Pia Dkt.Chuwa amesema kuwa kwa mjibu wa takwimu za umoja wa mataifa za mwaka 2017, dunia ikadiliwa kuwa na watu wapatao bilioni 7.53, Afrika bilioni 1.25 nchi zikizo kusini mwa jangwa la sahara bilioni 1.02 na kwa makadilio ya sensa ya mwaka 2012 na kwa kuzingatia viwango vya uzazi na vifo kwa takwimu za mwaka 2016, Tanzania inakadiliwa kuwa na idadi ya watu wapatao milioni 54.2 ambapo Tanzania bara ni milioni 52.6 na Zanzibar milioni 1.6 kwa mwaka 2018 hivyo idadi hiyo inakadiliwa kufikia watu milioni 59.4 ifikapo mwaka 2021 na kufikia mwaka 2030 idadi ya watu itafikia milioni 77.5.
Aidha mwakilishi wa umoja wa mataifa UNFPA Jackiline Moha amesema kuwa si Tanzania tu yenye kasi ya ongezeko la watu hali iko hivyo hata kwa nchi nyingine duniani kote na kuongeza kuwa kwa Tanzania 44% ya watu ni vijana wenye umri chini ya miaka 15 hivyo wakiangaliwa toka Kipindi cha ukuaji wao watakuwa na mchango mkubwa kwa taifa hasa kwa vijana wa kike hivyo serikali inatakiwa kufanya uwekezaji sahihi na kwa wakati sahihi kwa vijana kwa kuwapatia elimu na afya bora.

No comments:

Post a Comment