Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles
Mlingwa akiwa katika banda la Idara ya Elimu kutoka Halmashauri ya
Wilaya ya Serengeti katika maadhimisho ya Mei Mosi kimkoa Wilayani
Serengeti.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Ndugu
Nurdin Babu akiongea jambo katika maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika
Kimkoa katika Wilaya ya Serengeti.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles
Mlingwa akiongea jambo katika maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika
Kimkoa katika Wilaya ya Serengeti.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa akiwa katika banda la mjasiliamali wa mafuta ya alizeti Bi. Fatma Shams.
Mkuu wa Mkoa wa Mara akiwa katika
banda la Hifadhi ya Taifa TANAPA katika maadhimisho ya Mei Mosi
yaliyofanyika Kimkoa katika Wilaya ya Serengeti.
………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles
Mlingwa amewakata wafanyakazi kutoa huduma bora kwa wananchi kama
yalivyo makusudi ya serikali ya awamu ya tano (Hapa Kazi Tuu)
Dk. Mlingwa amesema hayo katika
maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kimkoa katika Wilaya ya
Serengeti siku ya jana tarehe 1 Mei 2017. Akikabidhi na kutunuku vyeti
kwa wafanyakazi bora; Mkuu wa Mkoa amesema “Wafanyakazi wasiwe mbele tuu
kupaza sauti kudai haki, pia wasimamie utendaji wao ambao unalalamikiwa
na wananchi.
Aidha licha ya mvua kubwa kunyesha
siku hiyo, haikuzuia kufana kwa sherehe hizo ambapo Mkuu huyo wa Mkoa
wa Mara ameipongeza Wilaya ya Serengeti kwa maandalizi mazuri ya Sherehe
hizo zilizoambatana na burudani, michezo pamoja na mabanda ya maonyesho
ya shughuli zifanywazo na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya Wilaya
Serengeti.
No comments :
Post a Comment