Pages

Tuesday, May 2, 2017

RC MARA AWATAKA WAFANYAKAZI KUTOA HUDUMA BORA

se1
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa akiwa katika banda la Idara ya Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti katika maadhimisho ya Mei Mosi kimkoa Wilayani Serengeti.
se2
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Ndugu Nurdin Babu akiongea jambo katika maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika Kimkoa katika Wilaya ya Serengeti.
se3
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa akiongea jambo katika maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika Kimkoa katika Wilaya ya Serengeti.
se4
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa akiwa katika banda la mjasiliamali wa mafuta ya alizeti Bi. Fatma Shams.
se5
Mkuu wa Mkoa wa Mara akiwa katika banda la Hifadhi ya Taifa TANAPA katika maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika Kimkoa katika Wilaya ya Serengeti.
………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa amewakata wafanyakazi kutoa huduma bora kwa wananchi kama yalivyo makusudi ya serikali ya awamu ya tano (Hapa Kazi Tuu)
Dk. Mlingwa amesema hayo katika maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kimkoa katika Wilaya ya Serengeti siku ya jana tarehe 1 Mei 2017. Akikabidhi na kutunuku vyeti kwa wafanyakazi bora; Mkuu wa Mkoa amesema “Wafanyakazi wasiwe mbele tuu kupaza sauti kudai haki, pia wasimamie utendaji wao ambao unalalamikiwa na wananchi.
Aidha licha ya mvua kubwa kunyesha siku hiyo, haikuzuia kufana kwa sherehe hizo ambapo Mkuu huyo wa Mkoa wa Mara ameipongeza Wilaya ya Serengeti kwa maandalizi mazuri ya Sherehe hizo zilizoambatana na burudani, michezo pamoja na mabanda ya maonyesho ya shughuli zifanywazo na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya Wilaya Serengeti.

No comments:

Post a Comment