Mkuu wa mkoa wa
Dodoma Jordan Rugimbana akimshukuru Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuondoka uwanja
wa ndege wa Dodoma kuelekea mkoani Kilimanjaro leo Aprili 29, 2017. Pamoja na
mambo mengine Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mei Mosi
zinazofanyika kitaifa mkoani humo (PICHA
NA IKULU)
SHAMIMU
NYAKI-WHUSM.
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto
(UNICEF) linaaanda mpango mkakati wa kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa
kulinda Haki za Watoto kwa kuandaa vipindi mbalimbali vya redio na luninga kama
njia ya haraka ya kufikisha ujumbe kwa jamii.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwakilishi
Mkazi
wa Shirika hilo hapa nchini Bi Maniza Zaman alipokutana na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe ambapo amesisitiza kuendeleza ushirikiano na Serikali katika Miradi na Programu za kulinda Watoto.
wa Shirika hilo hapa nchini Bi Maniza Zaman alipokutana na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe ambapo amesisitiza kuendeleza ushirikiano na Serikali katika Miradi na Programu za kulinda Watoto.
“UNICEF itaendelea kuandaa vipindi vya luninga na
redio kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda haki za
watoto ili itambue watoto wanahitaji nini katika maisha yao ya kujenga Taifa la
kesho” Alisema Bi Maniza.
Kwa upande wake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kutoa ushrikiano kwa UNICEF katika
mpango huo ambao una malengo ya kusaidia watoto kutambua haki zao
ikiwemo haki ya kupata taarifa.
“Watoto ndio viongozi wa kesho hivyo ni vyema
kuwalinda na kuwapatia haki zao wanazostahili ikiwemo ya kuwapa taarifa sahihi
na kwa wakati sahihi ili kuwajengea Utamaduni wa kupenda kuwasilisha mawazo
yao”.Alisema Mhe.Mwakyembe.
Aidha Mhe. Waziri Mwakyembe amevitaka vyombo vya
habari kutoa ushirikiano kwa UNICEF wakati itakapowasilisha vipindi hivyo vya
kuelimisha kuhusu haki za watoto ili wananchi wapate elimu itakayosaidia kutoa
malezi yanayostahili kwa watoto wao.
Mazungumzo hayo pia yamelenga kuimarisha ushirikiano
katika Sekta za Sanaa na Utamaduni zilizopo Chini ya Wizara kwa
lengo la kutambua fursa zinazoweza kutumika kwa manufaa ya pande mbili hizo.
No comments :
Post a Comment