2 FEBRUARY 2017 – NGOME KONGWE,
ZANZIBAR: Alhamis ya wiki ijayo tarehe 9 Februari tamasha la Sauti za
Busara litaanza na sekta ya utalii ndani ya Zanzibar itachukua sura
mpya. Baada ya mwaka mmoja wa kutofanyika kwa tamasha hilo, sasa tamasha
limerudi kuutangaza utamaduni, kujenga uwezo na kukuza uchumi wa ndani
pamoja na kutoa ajira na mafunzo kwa watu wa Afrika Mashariki.
Tamasha la Sauti za Busara
limetengeneza zaidi ya dola 70 za kimarekani kwenye pato la Zanzibar
tangu limeanza mwaka 2004. Kila mwaka, timu ya watu 10 huongezeka
kufikia watu 150 ambao huajiriwa kufanya kazi kwa ajili ya tamasha na
kipaumbele hutolewa kwa wazawa kwenye upande wa kusimamia mambo ya
wasanii, utawala, mahusiano ya habari, tiketi, vibanda vya mauzo na
ulinzi.
Lengo la Busara kutoa mafunzo na ujuzi ni kukuza uchumi wa jamii
ya ndani. Mwaka 2016 Busara Promotions ilitoa mafunzo juu ya usimamizi
wa jukwaa, ufundi wa sauti, usimamizi wa mwanga jukwaani, mambo ya
habari na ujuzi wa masoko. Kwa ushirikiana na matamasha kama Bushfire
huko Swaziland na Oya huko Norway, timu ya Busara imefaidika na
kubadilishana ujuzi na maswasiliano na timu za matamasha mengine.
Sauti za Busara imeseadia kuiweka
Zanzibar kwenye ramani ya utalii. Trish Dhanak, mmiliki wa Upendo hotel
anafafanua, “Kama muwekezaji, ni wajibu wetu kuwaonesha wasafiri uzuri
wa Zanzibar, na kujifunza kwa kina uhalisia wa kisiwa hiki. Sauti za
Busara ni kiunganisho kwa wasafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani na
Afrika ni muziki Zanzibar na ni matarajio yetu kuwa wakati wa uwepo wao
wata[ata sababu ya kuwafanya warudi.”
Kwa sasa Februari ni mwezi
ulio juu kwa kuwasili wageni zaidi ya elfu 40,000. Mpaka sasa huduma za
usafiri nyingi zimejaa. Hoteli na migahawa yote ishakuwa tayari
kuelekeza nguvu kuhudumia wageni wa tamasha,
Kadri tamsha linavyokua na
kuvutia wageni wengi wa kimataifa kila mwaka tunafanya tamasha kuwa
kipaumbele kwa wazawa. Mwaka huu, kwa watanzania tu kwa siku zote nne ni
Sh 20,000 au Sh6,000 kwa siku, Wenye asi za kusafiria za Afrika
watalipa Sh120,000 au Sh50,000 kwa siku. Tiketi zitapatikana Ngome
Kongwe kuanzia Jumanne tarehe 7 February, kuanzia saa 4:00 kamili
asubuhi.
Tamasha la Sauti za Busara 2017 limedhaminiwa na: Ubalozi wa Norway, Hirika la Uswis la Ushirikiana na Maendeleo
(SDC), ZANTEL, Africalia, Ubalozi wa Ujerumani, Zanlink, Memories of
Zanzibar, Ethiopian Airlines, Mozeti, Coastal Aviation, Ikala Zanzibar
Stone Town Lodge, Music in Africa, Chuchu FM Radio, Tifu TV na Zanzibar Media Corporation.
No comments :
Post a Comment