Pages

Thursday, February 2, 2017

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA LINAKUZA UTAMADUNI WA UTALII


BUSARA
2 FEBRUARY 2017 – NGOME KONGWE, ZANZIBAR: Alhamis ya wiki ijayo tarehe 9 Februari tamasha la Sauti za Busara litaanza na sekta ya utalii ndani ya Zanzibar itachukua sura mpya. Baada ya mwaka mmoja wa kutofanyika kwa tamasha hilo, sasa tamasha limerudi kuutangaza utamaduni, kujenga uwezo na kukuza uchumi wa ndani pamoja na kutoa ajira na mafunzo kwa watu wa Afrika Mashariki.
Tamasha la Sauti za Busara limetengeneza zaidi ya dola 70 za kimarekani kwenye pato la Zanzibar tangu limeanza mwaka 2004. Kila mwaka, timu ya watu 10 huongezeka kufikia watu 150 ambao huajiriwa kufanya kazi kwa ajili ya tamasha na kipaumbele hutolewa kwa wazawa kwenye upande wa kusimamia mambo ya wasanii, utawala, mahusiano ya habari, tiketi, vibanda vya mauzo na ulinzi.

Lengo la Busara kutoa mafunzo na ujuzi ni kukuza uchumi wa jamii ya ndani. Mwaka 2016 Busara Promotions ilitoa mafunzo juu ya usimamizi wa jukwaa, ufundi wa sauti, usimamizi wa mwanga  jukwaani, mambo ya habari na ujuzi wa masoko. Kwa ushirikiana na matamasha kama Bushfire huko Swaziland na Oya huko Norway, timu ya Busara imefaidika na kubadilishana ujuzi na maswasiliano na timu za matamasha mengine.

Sauti za Busara imeseadia kuiweka Zanzibar kwenye ramani  ya utalii. Trish Dhanak, mmiliki wa Upendo hotel anafafanua, “Kama muwekezaji, ni wajibu wetu kuwaonesha wasafiri uzuri wa Zanzibar,  na kujifunza  kwa kina uhalisia wa kisiwa hiki.   Sauti za Busara ni kiunganisho kwa wasafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani na Afrika ni muziki Zanzibar na ni matarajio yetu kuwa wakati wa uwepo wao wata[ata sababu ya kuwafanya warudi.”
Kwa sasa Februari ni mwezi ulio juu kwa kuwasili wageni zaidi ya elfu 40,000. Mpaka sasa huduma za usafiri nyingi zimejaa. Hoteli na migahawa yote ishakuwa tayari kuelekeza nguvu kuhudumia wageni wa tamasha,
Kadri tamsha linavyokua na kuvutia wageni wengi wa kimataifa kila mwaka tunafanya tamasha kuwa kipaumbele kwa wazawa. Mwaka huu, kwa watanzania tu kwa siku zote nne ni Sh 20,000 au Sh6,000 kwa siku, Wenye asi za kusafiria za Afrika watalipa Sh120,000 au Sh50,000 kwa siku. Tiketi zitapatikana Ngome Kongwe kuanzia Jumanne tarehe 7 February, kuanzia saa 4:00 kamili asubuhi.
Tamasha la Sauti za Busara 2017 limedhaminiwa na: Ubalozi wa Norway, Hirika la Uswis la Ushirikiana na Maendeleo  (SDC), ZANTEL, Africalia, Ubalozi wa Ujerumani, Zanlink, Memories of Zanzibar, Ethiopian Airlines, Mozeti, Coastal Aviation, Ikala Zanzibar Stone Town Lodge, Music in Africa, Chuchu FM Radio, Tifu TV na Zanzibar Media Corporation.

No comments:

Post a Comment