Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji
wa Bunda Bi. Janeth Mayanja amemvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Bunda B, Bw. Laurent Agustino kwa tuhuma za kushiriki kusaidia
mwanafunzi mmoja kufanya udanganyifu katika mtihani wa darasa la nne.
Mwalimu huyo anatuhumiwa kumruhusu
mwanafunzi wa darasa la tano kufanyia mtihani wa mwanafunzi wa darasa
nne kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi huyo ambaye hajui kusoma wala
kuandika ili aweze kufaulu.
Mkurugenzi huyo ametoa kauli hiyo leo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi.
Kufuatia tukio hilo Bi. Janeth
ametoa onyo kwa walimu wote wa shule zilizofanya vibaya na kuwataka
kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani kwa mwaka 2017 na kuahidi
kuwavua madaraka walimu wa shule zitakazofanya vibaya.
Aidha, Mkurugenzi huyo wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda amewataka walimu wakuu, waratibu na
walimu wote kutekeleza kutekeleza majukumu yao kulingana na sheria na
kanun9 a utumishi wa Umma.
Mkurugenzi huyo amezizawadia
shule kumi za Msingi zilizofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza
Darasa la saba kwa mwaka 2016 kwa ajili ya kuboresha kiwango cha elimu
katika eneo hilo.
Utaratibu huo ulenga kutoa hamasa
kwa wanafunzi na walimu wilayani humo na kuongeza juhudi katika
kufundisha na kujifunza kwa ajili ya kuongeza kiwango cha ufaulu katika
Halmashauri hiyo.
Amezitaja shule zilizoingia kumi
bora ni pamoja na Olympus, Daystar, St. Paul, Mzuma, Kabarimu B, Bigutu,
Bukore, Kung’ombe, Kabarimu A na Bitaraguru ambazo zote zimetunukiwa
vyeti vya kutambua mchango na juhudi wanazofanya.
Mayanja alisema kuwa kati ya shule
hizo nne ni shule binafsi na sita za Serikali ambazo ambapo pamoja
na zimekabidhiwa hundi za fedha.
No comments:
Post a Comment