Na Anthony John Glob Jamii.
MKUU wa mkoa wa Dar es salaam
Paul Makonda amewataja baadhi ya Maafisa wa Jeshi la polisi wanao
shirikiana na Wasanii wanaojihusisha na uuzwaji wa dawa za kulevya.
Akizungumza na waandishi wa
Habari mapema leo hii jijini hapa amesema Serikali ya awamu ya Tano
haito vumilia vitendo vya uuzwaji wa dawa za kulevya na kutoa agizo kwa
jeshi la polisi kuwakamata Maafisa wote wa jeshi la polisi waliotajwa
kushirikiana na wauza madawa ya kulevya mpaka pale uchunguzi utakapo
kamilika.
” nimepata taarifa kuwa baadhi
ya Askari wa Jeshi polisi wanajihusisha na uuzwaji wa madawa ya kulevya
na wengine wamekuwa na utaratibu wa kwenda kuchukua pesa kila juma mosi
kwa wauzaji wa madawa ya kulevya na ndio maana biashara hii inaendelea
kuwepo kwakuwa wanashirikiana na wauzaji” amesema Makonda.
Wakati huo huo Makonda
amewataka wale wote waliotajwa kuhusika na kuuza dawa za kulevya
wanatakiwa kufika katika kituo cha polisi kati kwaajili ya mahojiano.
No comments :
Post a Comment