Pages

Thursday, February 2, 2017

MAKONDA ATAJA MAJINA YA WAUZA DAWA ZA KULEVYA.


Makonda
 Na Anthony John Glob Jamii.
MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataja baadhi ya Maafisa wa Jeshi la polisi wanao shirikiana na Wasanii wanaojihusisha na uuzwaji wa dawa za kulevya.
 Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo hii jijini hapa amesema Serikali ya awamu ya Tano haito vumilia vitendo vya uuzwaji wa dawa za kulevya na kutoa agizo kwa jeshi la polisi kuwakamata Maafisa wote wa jeshi la polisi waliotajwa kushirikiana na wauza madawa ya kulevya mpaka pale uchunguzi utakapo kamilika.
 ” nimepata taarifa kuwa baadhi ya Askari wa Jeshi polisi wanajihusisha na uuzwaji wa madawa ya kulevya na wengine wamekuwa na utaratibu wa kwenda kuchukua pesa kila juma mosi kwa wauzaji wa madawa ya kulevya na ndio maana biashara hii inaendelea kuwepo kwakuwa  wanashirikiana na wauzaji” amesema Makonda.
  Wakati huo huo Makonda  amewataka wale wote waliotajwa kuhusika na kuuza dawa za kulevya wanatakiwa kufika katika kituo cha polisi  kati kwaajili ya mahojiano.

No comments:

Post a Comment