Wednesday, November 2, 2016

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA


MWAMUZI WA KIKE TANZANIA KUCHEZESHA AFCON YA KINAMAMA


KIOTA KIPYA ,BENDI MPYA YA MJENGONI VYWAZINDULIWA RASMI JIJINI ARUSHA MAMIA WAJITOKEZA KWEYE UZINDUZI HUO

Mkurugenzi wa mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John Mdeme akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi huo
  Wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa mjengoni klabu pamoja na mjengoni band wakiwa wanaagiza nyama kwa ajili ya kula(habari pich na Woinde Shizza)
 Bendi mpya inayojulikana kama Mjengoni bandi ikiwa inatumbuiza wageni waalikwa , washabiki pamoja na wananchi waliouthuria katika uzinduzi huo
 mashabiki na wapenzi wa bendi ya mjengoni wakiwa wanasakata rumba hatariii

WAFANYAKAZI WA SHAMBA LA MIPIRA KICHWELE WAIOMBA SMZ IWARUHUSU KULIENDELEZA BAADA YA AGRO TEC KUSHINDWA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za huduma za Umma{ ZAPSWU } Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.  Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Chama cha ZAPSWU Nd. Nd.Ameir Mwadini na kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Bibi Mwatum Othman.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar { ZAPSWU } Bibi Mwatum Othman aliyesimama akitoa ufafanuzi katika Kikao cha mrejesho wa agizo la Balozi Seif aliloupa Uongozi huo mnamo Tarehe 9 Juni mwaka 2016 wa kukutana na Wizara ya Fedha kuangalia namna ya kulitafutia ufumbuzi wa shamba la mipira Kichwele.
Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar Nd. Ameir Mwadini.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar { ZAPSWU } wakifuatilia mazungumzo yao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.

                                                                                                    Picha na – OMPR – ZNZ.
 

Wafanyakazi wa shamba ya mipira Kichwele liliopo Wilaya ya Kaskazini “B” wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuandaa utaratibu utakaowapa idhini ya kulihudumia shamba hilo kiuzalishaji baada ya Kampuni iliyopewa jukumu la kuliendesha shamba hilo ya Agro Tec kushindwa kuliendeleza.

Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za huduma za Umma{ ZAPSWU } Tawi la Shamba hilo Bibi Kazija Sheha Mohammed alitoa ombi hilo wakati Uongozi wa Chama hicho Taifa ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kufanya mrejesho wa agizo aliloupa mnamo Tarehe 9 Juni mwaka 2016 wa kukutana na Wizara ya Fedha kuangalia namna ya kulitafutia ufumbuzi wa shamba hilo.

Bibi Kazija alisema wafanyakazi wa shamba la mipira Kichwele kwa sasa wanaendelea kukabiliwa na ukali maisha kufuatia Uongozi wa Kampuni ya Agro Tek kusitisha uzalishaji wa mipira uliokwenda sambamba na kulimbikiza madeni ya mishahara ya muda mrefu ya wafanyakazi hao.

Alisema endapo Serikali Kuu itaridhia ombi lao upo uwezekano mkubwa kwa ari waliokuwa nayo wafanyakazi hao kuliendeleza shamba hilo kwa nia ya kutafuta faraja ya kupunguza changamoto za muda mrefu zinazowakabili katika mradi huo wa uwekezaji.

Alieleza kwamba changamoto kama hiyo kwa wafanyakazi wenzao wa Kisiwa cha Pemba imeshapatiwa ufumbuzi baada ya Uongozi wa Mkoa kuwapa ruhusa ya kuendeleza mradi huo ili kukidhi mahitaji yao.

ubal
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akijibu hoja iliyohusu mpango wa Tanzania kufungua ubalozi mdogo nchini China katika kikao cha pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma.
………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imejipanga kufungua ofisi ya ubalozi mdogo katika mji wa Guangzhou uliyopo nchini China ili kongeza fursa za kibiashara pamoja na kurahisisha huduma mbalimbali Watanzania wanaoishi nchini humo.
Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Suzan Kolimba alipokuwa akijibu swali la Mhe. Machano Said aliyehoji juu ya kuwekwa kwa ubalozi wa Tanzania nchini China pamoja na utaratibu unaotumika katika kuwapa Visa wananchi ambao wameaamua kuishi nchini humo.
Mhe. Dkt Kolimba amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali ya China kuchagua majimbo matatu ya Jiangsu, Zhejiang pamoja na Guangdong ili yawe na uhusiano maalum na nchi tatu za Afrika ambapo Tanzania ni moja ya nchi hizo.
“Tunaamini kuwa kwa kufungua ofisi za ubalozi katika mji huu Tanzania itakuwa na fursa ya kuyashawishi makampuni ya mji huo kuja kuwekeza katika nchi yetu pamoja na kutoa huduma mbalimbali kwa Watanzania wanaofanya biashara katika mji huo”, alisema Dkt. Kolimba.
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa mahusiano ya kimataifa ni njia mojawapo ya kuimarisha shughuli za kibiashara na kijamii miongoni mwa wananchi wa nchi hizo mbili katika kuwaletea maendeleo. 
Akiongelea kuhusu Watanzania walioamua kuishi nchini china, Dkt Kolimba amebainisha kuwa utaratibu uliopo sasa kwa wananchi wanaoishi zaidi ya mwaka mmoja katika nchi hiyo wanatakiwa kuwa na kibali cha kuishi nchini humo.
Aidha, Dkt. Kolimba amefafanua kuwa kibali hicho kinapatikana kwa kuwasilisha maombi kwenye wizara inayoshughulika na masuala ya mambo ya ndani ya China na iwapo watakuwa wamekidhi vigezo vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi hiyo watapatiwa vibali hivyo. 

BILIONI 3 KUKARABATI MAGEREZA NCHINI

unnamednn
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma.
……….
              Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma
 
Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3 katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kukarabati, kupanua na kumalizia ujenzi wa mabweni mapya pamoja na majengo ya utawala katika baadhi ya magereza nchini.  
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba ameyathibitisha hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe. Hawa Mwaifunga (Mbunge wa Viti Maalumu) lililohoji kuhusu mpango wa Serikali katika kuhakikisha hali za magereza katika Mkoa wa Tabora zinaboreshwa.
Mhe. Mwigulu amesema kuwa katika kuhakikisha hali ya magereza nchini inaboreshwa ili kuhakikisha haki za binadamu zinatekelezwa, Serikali inaendelea na mpango endelevu wa kufanya upanuzi wa magereza ya zamani na kujenga magereza mapya katika kila Wilaya ambapo utekelezaji huo unafanyika kulingana na upatikanaji wa fedha.
“Katika mwaka huu wa fedha, Serikali imetenga bilioni 3 katika Bajeti kupitia Fungu la Maendeleo kwa ajili ya kukarabati magereza ambapo shilingi milioni 185 kati ya bajeti iliyotengwa ni kwa ajili ya kukarabati magereza ya Mkoa wa Tabora, hivyo tunategemea magereza ya mkoa huo yatakuwa katika hali nzuri”, amesema Mwigulu.
Ameongeza kuwa Serikali inatambua msongamano wa mahabusu uliopo katika magereza mengi nchini na kuongeza kuwa Jukwaa la Haki Jinai limekuwa likifanya vikao vya kuharakisha kesi ambazo upelelezi wake haujakamilika ili kupunguza msongamano huo.
Aidha, Waziri Mwigulu amesema kuwa Serikali inahakikisha Askari Wapelelezi wanapewa mafunzo kulingana na kazi yao ili waweze kufanya ukamataji wa watuhumiwa kwa kuzingatia uzito wa ushahidi wa muhusika na kuepusha malalamiko ya kubambikiwa kesi na kujikuta Serikali inatumia gharama nyingi kuwatunza mahabusu hao.
Kuhusu usalama wa askari, Waziri Mwigulu amesema kuwa Serikali itaendelea kuliwezesha Jeshi la Polisi nchini kwa kuwapa vitendea kazi bora na kuwajengea uwezo wa mafunzo askari hao ili waweze kukabiliana na matukio ya uhalifu dhidi ya wanananchi na mali zao pamoja na uvamizi wa vituo vya polisi nchini.
“Hadi kufikia Septemba 2016 Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha 19 kati ya 23 zilizoporwa kutoka kwa askari waliovamiwa wakiwa wakitekeleza majukumu yao hatua inayoonesha jeshi la Polisi linavyofanya kazi kwa umakini” alisema Mwigulu.
Kwa upande mwingine, Waziri Mwigulu ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa katika vituo vya Polisi vilivyo karibu pindi wanapokuwa na shaka juu ya watu wasiowatambua au kufanya kazi zisizoeleweka ili kuwahakikishia wananchi usalama wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kimaendeleo.

No comments :

Post a Comment