KIOTA KIPYA ,BENDI MPYA YA MJENGONI VYWAZINDULIWA RASMI JIJINI ARUSHA MAMIA WAJITOKEZA KWEYE UZINDUZI HUO
Mkurugenzi wa mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John Mdeme akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi huo
Wadau
waliojitokeza katika uzinduzi wa mjengoni klabu pamoja na mjengoni band
wakiwa wanaagiza nyama kwa ajili ya kula(habari pich na Woinde Shizza)
Bendi
mpya inayojulikana kama Mjengoni bandi ikiwa inatumbuiza wageni
waalikwa , washabiki pamoja na wananchi waliouthuria katika uzinduzi huo
mashabiki na wapenzi wa bendi ya mjengoni wakiwa wanasakata rumba hatariii
WAFANYAKAZI WA SHAMBA LA MIPIRA KICHWELE WAIOMBA SMZ IWARUHUSU KULIENDELEZA BAADA YA AGRO TEC KUSHINDWA
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi
wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za huduma za Umma{ ZAPSWU } Ofisini
kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Chama
cha ZAPSWU Nd. Nd.Ameir Mwadini na kushoto ya Balozi Seif ni Katibu
Mkuu wa Chama hicho Bibi Mwatum Othman.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar {
ZAPSWU } Bibi Mwatum Othman aliyesimama akitoa ufafanuzi katika Kikao
cha mrejesho wa agizo la Balozi Seif aliloupa Uongozi huo mnamo Tarehe 9
Juni mwaka 2016 wa kukutana na Wizara ya Fedha kuangalia namna ya
kulitafutia ufumbuzi wa shamba la mipira Kichwele.
Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar Nd. Ameir Mwadini.
Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar Nd. Ameir Mwadini.
Baadhi
ya Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma
Zanzibar { ZAPSWU } wakifuatilia mazungumzo yao na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif.
Wafanyakazi wa shamba ya mipira Kichwele liliopo Wilaya ya Kaskazini “B” wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuandaa utaratibu utakaowapa idhini ya kulihudumia shamba hilo kiuzalishaji baada ya Kampuni iliyopewa jukumu la kuliendesha shamba hilo ya Agro Tec kushindwa kuliendeleza.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za huduma za Umma{ ZAPSWU } Tawi la Shamba hilo Bibi Kazija Sheha Mohammed alitoa ombi hilo wakati Uongozi wa Chama hicho Taifa ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kufanya mrejesho wa agizo aliloupa mnamo Tarehe 9 Juni mwaka 2016 wa kukutana na Wizara ya Fedha kuangalia namna ya kulitafutia ufumbuzi wa shamba hilo.
Bibi Kazija alisema wafanyakazi wa shamba la mipira Kichwele kwa sasa wanaendelea kukabiliwa na ukali maisha kufuatia Uongozi wa Kampuni ya Agro Tek kusitisha uzalishaji wa mipira uliokwenda sambamba na kulimbikiza madeni ya mishahara ya muda mrefu ya wafanyakazi hao.
Alisema endapo Serikali Kuu itaridhia ombi lao upo uwezekano mkubwa kwa ari waliokuwa nayo wafanyakazi hao kuliendeleza shamba hilo kwa nia ya kutafuta faraja ya kupunguza changamoto za muda mrefu zinazowakabili katika mradi huo wa uwekezaji.
Alieleza kwamba changamoto kama hiyo kwa wafanyakazi wenzao wa Kisiwa cha Pemba imeshapatiwa ufumbuzi baada ya Uongozi wa Mkoa kuwapa ruhusa ya kuendeleza mradi huo ili kukidhi mahitaji yao.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki akijibu hoja iliyohusu mpango wa Tanzania kufungua
ubalozi mdogo nchini China katika kikao cha pili cha Bunge la 11 la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma.
………………………………………………………………..
………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma
Serikali
kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
imejipanga kufungua ofisi ya ubalozi mdogo katika mji wa Guangzhou
uliyopo nchini China ili kongeza fursa za kibiashara pamoja na
kurahisisha huduma mbalimbali Watanzania wanaoishi nchini humo.
Hayo
yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Suzan
Kolimba alipokuwa akijibu swali la Mhe. Machano Said aliyehoji juu ya
kuwekwa kwa ubalozi wa Tanzania nchini China pamoja na utaratibu
unaotumika katika kuwapa Visa wananchi ambao wameaamua kuishi nchini
humo.
Mhe.
Dkt Kolimba amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali ya
China kuchagua majimbo matatu ya Jiangsu, Zhejiang pamoja na Guangdong
ili yawe na uhusiano maalum na nchi tatu za Afrika ambapo Tanzania ni
moja ya nchi hizo.
“Tunaamini
kuwa kwa kufungua ofisi za ubalozi katika mji huu Tanzania itakuwa na
fursa ya kuyashawishi makampuni ya mji huo kuja kuwekeza katika nchi
yetu pamoja na kutoa huduma mbalimbali kwa Watanzania wanaofanya
biashara katika mji huo”, alisema Dkt. Kolimba.
Naibu
Waziri huyo ameongeza kuwa mahusiano ya kimataifa ni njia mojawapo ya
kuimarisha shughuli za kibiashara na kijamii miongoni mwa wananchi wa
nchi hizo mbili katika kuwaletea maendeleo.
Akiongelea
kuhusu Watanzania walioamua kuishi nchini china, Dkt Kolimba
amebainisha kuwa utaratibu uliopo sasa kwa wananchi wanaoishi zaidi ya
mwaka mmoja katika nchi hiyo wanatakiwa kuwa na kibali cha kuishi nchini
humo.
Aidha,
Dkt. Kolimba amefafanua kuwa kibali hicho kinapatikana kwa kuwasilisha
maombi kwenye wizara inayoshughulika na masuala ya mambo ya ndani ya
China na iwapo watakuwa wamekidhi vigezo vinavyotakiwa kwa mujibu wa
sheria na taratibu za nchi hiyo watapatiwa vibali hivyo.
BILIONI 3 KUKARABATI MAGEREZA NCHINI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha
pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini
Dodoma.
……….
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma
Serikali
imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3 katika Bajeti ya mwaka wa fedha
2017/2018 kwa ajili ya kukarabati, kupanua na kumalizia ujenzi wa
mabweni mapya pamoja na majengo ya utawala katika baadhi ya magereza
nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba ameyathibitisha hayo
leo mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe. Hawa Mwaifunga (Mbunge
wa Viti Maalumu) lililohoji kuhusu mpango wa Serikali katika kuhakikisha
hali za magereza katika Mkoa wa Tabora zinaboreshwa.
Mhe.
Mwigulu amesema kuwa katika kuhakikisha hali ya magereza nchini
inaboreshwa ili kuhakikisha haki za binadamu zinatekelezwa, Serikali
inaendelea na mpango endelevu wa kufanya upanuzi wa magereza ya zamani
na kujenga magereza mapya katika kila Wilaya ambapo utekelezaji huo
unafanyika kulingana na upatikanaji wa fedha.
“Katika
mwaka huu wa fedha, Serikali imetenga bilioni 3 katika Bajeti kupitia
Fungu la Maendeleo kwa ajili ya kukarabati magereza ambapo shilingi
milioni 185 kati ya bajeti iliyotengwa ni kwa ajili ya kukarabati
magereza ya Mkoa wa Tabora, hivyo tunategemea magereza ya mkoa huo
yatakuwa katika hali nzuri”, amesema Mwigulu.
Ameongeza
kuwa Serikali inatambua msongamano wa mahabusu uliopo katika magereza
mengi nchini na kuongeza kuwa Jukwaa la Haki Jinai limekuwa likifanya
vikao vya kuharakisha kesi ambazo upelelezi wake haujakamilika ili
kupunguza msongamano huo.
Aidha,
Waziri Mwigulu amesema kuwa Serikali inahakikisha Askari Wapelelezi
wanapewa mafunzo kulingana na kazi yao ili waweze kufanya ukamataji wa
watuhumiwa kwa kuzingatia uzito wa ushahidi wa muhusika na kuepusha
malalamiko ya kubambikiwa kesi na kujikuta Serikali inatumia gharama
nyingi kuwatunza mahabusu hao.
Kuhusu
usalama wa askari, Waziri Mwigulu amesema kuwa Serikali itaendelea
kuliwezesha Jeshi la Polisi nchini kwa kuwapa vitendea kazi bora na
kuwajengea uwezo wa mafunzo askari hao ili waweze kukabiliana na matukio
ya uhalifu dhidi ya wanananchi na mali zao pamoja na uvamizi wa vituo
vya polisi nchini.
“Hadi
kufikia Septemba 2016 Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha 19
kati ya 23 zilizoporwa kutoka kwa askari waliovamiwa wakiwa wakitekeleza
majukumu yao hatua inayoonesha jeshi la Polisi linavyofanya kazi kwa
umakini” alisema Mwigulu.
Kwa
upande mwingine, Waziri Mwigulu ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa
katika vituo vya Polisi vilivyo karibu pindi wanapokuwa na shaka juu ya
watu wasiowatambua au kufanya kazi zisizoeleweka ili kuwahakikishia
wananchi usalama wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment