Monday, August 29, 2016

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AHUDHURIA KIKAO CHA SADC TROIKA MJINI MBABANE SWAZILAND


 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijianda na mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika umefanyika mchana huu  katika ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipata maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi na Balozi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shio (katikati) kulia ni Waziri Mambo ya Njena ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) muda mfupi kabla ya kuanza kwa  Mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika umefanyika mchana huu  katika ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.

 Hii ndio muonekano wa Ukumbi wa Mkutano wa Mandvulo Grand uliopo Lozitha mjini Mbabane Swaziland ambapo mkutano wa 36 SADC unafanyika.
                                    
Mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika umefanyika mchana huu  katika ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.

Mkutano huo wa Troika unaohusisha nchi Tatu ambazo ni za Utatu ikiwemo Tanzania, Msumbiji na Afrika Kusini ambapo kwa kuzingatia utaratibu huo mkutano huo unahudhuriwa na Wakuu wa nchi na serikali wa Msumbiji kama Mwenyekiti wa Asasi hiyo (SADC Organ Troika Summit) na Afrika Kusini kama mwenyekiti aliyetoka na Tanzania inatarajiwa kukabidhi uenyekiti wa Asasi hiyo.

Baadhi ya ajenda ambazo viongozi hao watajadili kwenye mkutano huo ni hali ya ulinzi na usalama katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Lesotho, masuala ya upatanishi na utatuzi wa migogoro pamoja na maombi ya Burundi na Comoro kutaka kujiunga katika Jumuiya ya Mandeleo Kusini mwa Afrika- SADC.
Katika mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Ufunguzi rasmi wa mkutano wa SADC utafanyika terehe 30-Aug-16 katika ukumbi wa  Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland ambapo pamoja na Mambo mengine mkutano huo utatoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda katika uandishi wa insha katika jumuiya hiyo.

MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA JWTZ, JKT MGULANI YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM


 Meja Dora Kawawa wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa 831 KJ Mgulani (kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula, Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, Dar es Salaam leo jioni , ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambapo kilele chake kitakuwa Septemba Mosi mwaka huu.
 Maofisa wa Jeshi wa kikosi hicho wakifurahi na watoto wa kituo hicho baada ya kutoa msaada wao.
 Msaada ukitolewa.
 Hapa ni furaha pamoja na watoto hao.
 Watoto wakipata msaada huo.
 Watoto wakipokea msaada.
 Hapa ni furaha tupu kwa watoto kwa kupokea msaada kutoka kwa wazazi wao hao.
Picha ya pamoja na watoto hao na viongozi wao.

Na Dotto Mwaibale

JESHI la Kujenga Taifa Kikosi 831 Kj Mgulani limetoa msaada wa vyakula na sabuni kwa watoto waishio Makao ya Taifa ya Watoto Wenye Shida Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo kwa niaba ya mkuu wa kikosi hicho Dar es Salam , Meja Dora Kawawa alisema ni moja ya sehemu ya maadhimisho ya kusherehekea miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

"Tumeamua kushiriki shughuli za kijamii kama kutoa msaada na kufanya usafi ikiwa ni kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa jeshi letu ambapo kilele chake kitakuwa Septemba mosi mwaka huu" alisema Kawawa.

Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance alishuru JKT kwa msaada huo na kueleza ni muhimu sana kwa watoto hao na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kujenga taifa bora la kesho.


 Wananchi wakiangalia ajali iliyosababishwa na daladala lenye namba za usajili T 397 BVB linalofanya safari zake kati ya Temeke na Gongo la Mboto kwa kuyagonga magari mengine matatu eneo la Maji Matitu Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo namba T 628 DFE alijeruhiwa.
 Gari dogo namba T 628 DFE lililogongwa na daladala hilo likiwa limeharibika.
 Daladala hiloegonga gari namba T 458 CAN.
 Kuku waliokuwa kwenye moja ya gari lililogongwa wakiondolewa kuku kadhaa walipoteza maisha katika ajali hiyo.
 Askari wa Usalama barabarani akiangalia ajali hiyo.
Daladala uso kwa uso na gari dogo.

Na Dotto Mwaibale

MKAZI wa Chamazi ambaye ni mwanamke amejeruhiwa baada ya gari lake dogo alilokuwa akiendesha kugongwa na daladala lenye namba T 397 BVB linadodaiwa kuiba njia.

Ajali hiyo imetokea Maji Matitu Temeke jijini Dar es Salaam leo  asubuhi ambapo daladala hilo pia liliyagonga magari mengine matatu na kuzua kizaazaa katika barabara ya Charambe kwenda Chamazi.

Mkazi wa eneo hilo Hamisi Juma aliyeshuhudia ajali hiyo amesema ni mungu kasaidia kutokea kwa vifo kwani ajali hiyo ilikuwa ni mbaya sana.

" Saa 12 na dakika 55 nikiwa nasubiri gari kwenda kazini niliona daladala lililokuwa likitoka Charambe kwenda Chamazi lilikuwa likipita upande ambao si wake likiwa katika mwendo wa kasi na ghafla lililigonga gari dogo namba T 628 DFE ambalo ligeuka na kulala katika mtaro" alisema Juma.

Alisema baada ya kuligonga gari hilo liliyaparamia magari mengine madogo mawili likiwepo lililobeba kuku na kuyasukumia kwenye mtaro.

Aliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo dereva wa daladala hilo alikimbia na kulitelekeza gari lake.

Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T 628 DFE, T 397 BVB, T 451 CQB na T 458 CAN.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ili kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokewa alipopigiwa simu mara kadhaa.




Mkuu wa wilaya ya Muleba  Bw Richard Ruyango , akifungua rasmi tamasha la Tigo fiesta kwenye uwanja wa David Zihimbile wilayani humo usiku wa jana, Kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya ziwa Edgar Mapande na kushoto mkurugenzi wa vipindi clouds Ruge Mutahaba na mwakilishi kutoka wilayani.

Msanii Christian Bella akipagawisha kwenye Tamasha la Tigo Fiesta wilaya Muleba usiku wa jana lililofanyika uwanja wa David Zihimbile.
Msanii Joh Makini akiwarusha mashabiki wa hip hop kwenye Tamasha la Tigo Fiesta wilaya Muleba usiku wa jana lililofanyika uwanja wa David Zihimbile.


 Meya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Boniface Jacob, (watatu kushoto), na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (wanne kushoto), wakiongozana na wananchi na baadhi yaviongozxi wa wilaya hiyo, wakati wa ziara ya kutembelea eneo la mgogoro huko Kunduchi Mecco Mji mpya jijini Dar es Salaam.



BARAZA Kuu la Uongozi la Chama Cha Wananchi CUF, lililoketi mjini Unguja Jumapili Agosti 28, 2016, limewasimamisha uanachama aliyekuwa Mswenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Magdalena Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa
Kaliua mkoani Tabora.
Katika taarifa yake kwa v yombo vya habari iliyotolewa leo Agosti 29, 2016 makao makuu ya chama hicho Vuga kisiwani Unguja, Viongozi hao pia watatakiwa kujieleza mbele ya baraza hilo kwa hatua zaidi.
Taarifa ya Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Nassor Ahmed Mazrui, alisema uamuzi wa kuwasimamisha uanachama viongozi hao umezingatia Katiba ya Chama, Ibara ya 83 (5)(c), hadi hapo watakapopata fursa ya kujieleza mbele ya Baraza Kuu
Pia Baraza hilo limetoa karipio kali kwa viongozi kadhaa, chini ya  Ibara ya 83 (5)(b) ambao ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa 1. Rukiya Kassim Ahmed na
2. Athumani Henku
Viongozi wengine waliosimamishwa uanachamasambamba na Profesa Lipumba na Sakaya ni pamoja na
3. Abdul Kambaya
4. Ashura Mustafa
5. Omar Mhina Masoud
6. Thomas Malima
7. Kapasha M. Kapasha
8. Maftaha Nachumu
9.Mohamed Habib Mnyaa
10. Haroub Shamis 
na
11. Mussa Haji Kombo
Mwanachama aliyefukuzwa chama ambaye alipata fursa ya kujieleza mbele ya Baraza Kuu na kikao kuamua kumfukuza chama kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 83 (5)(c) ni aliyekuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wazee wa CUF (JUWACUF), Shashu Lugeye.
Kufuatia maamuzi hayo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limewateua viongozi mbali mbali kukaimu nafasi mbali mbali zilizoachwa wazi.
Kwa kuzingatia kwamba kutokamilika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa tarehe 21 Agosti, 2016 kulipelekea kushindwa kufanyika kwa uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limetumia uwezo liliopewa na Katiba ya Chama, Ibara ya 101 na 118, kuunda Kamati ya Uongozi ambayo itakuwa ikifanya kazi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti hadi hapo uchaguzi wa kujaza nafasi hizo utakapofanyika. Baraza Kuu la Uongozi limewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati hiyo ya Uongozi:
1. Mhe. Julius Mtatiro – Mwenyekiti;
2. Mhe. Katani Ahmed Katani – Mjumbe; na
3. Mhe. Severina Mwijage – Mjumbe.
Aidha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, kwa kufuata Ibara ya 105 (1) na (3) ya Katiba ya Chama, limemteua Mhe. Joran Bashange kuwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Chama kwa upande wa Tanzania Bara na Mhe. Mbarala Maharagande kuwa Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma hadi hapo nafasi hizo zitakapojazwa rasmi kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Chama.
Mwisho, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawahakikishia wanachama na wapenzi wake na Watanzania wote kwa ujumla kuwa Chama Cha Wananchi – CUF kipo imara na makini na katu hakitoyumbishwa kwa hila na njama ovu na chafu zinazofanywa na maadui wa chama hichi. Tangu kuasisiwa kwake, CUF imeandamwa na maadui wa kila aina, na imepitia katika misuko suko mingi. Tunaamini hila na njama hizo ovu zimekuwa zikielekezwa CUF kwa kutambua kwamba Chama hichi ndicho kinachobeba dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kweli hapa nchini.
Kutokana na umadhubuti, umakini na uimara wa Katiba ya Chama na safu ya viongozi wake, CUF imeweza kuvuka salama kila ilipoingia katika misuko suko hiyo na kwa hivyo, hata wimbi hili lililoonekana kukitikisa Chama limekabiliwa ipasavyo na sasa kazi iliyopo mbele yetu ni kuendeleza harakati za kisiasa za kuwaletea Watanzania wa Bara na Zanzibar mabadiliko wanayoyataka.


Mgeni Rasmi Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma kwa Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi. Wengine ni Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango (kushoto) na Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, Lorah Madete, akitoa neno kwa Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi ambao ni washiriki wa mafunzo yanayohusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili afungue mafunzo hayo ya siku tano.  Waliokaa ni Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (katikati) na Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Washiriki wa Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma ambao ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika Mkoani Tabora.


Washiriki wa Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma ambao ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika Mkoani Tabora.

Picha ya pamoja

(PICHA ZOTE NA: THOMAS NYINDO-TUME YA MIPANGO)

Wakazi wa Boko jijini Dar es Salaam wakihangaika kucheza muziki wa Singeli kwenye tamasha la Muziki Mnene lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania.Tamasha hilo lililoanza jijini Dar  es Salaam eneo la Boko mwishoni mwa wiki, litaendelea katika mkoani ya Pwani


Msaanii wa Muziki wa Singeli, Machupa akikonga mioyo ya wapenzi wa muziki huo kwenye tamasha la Muziki Mnene lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania.Tamasha hilo lililoanza jijini Dar  es Salaam eneo la Boko mwishoni mwa wiki, litaendelea katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.



Wakazi wa Boko jijini Dar es Salaam wakihangaika kucheza muziki wa Singeli kwenye tamasha la Muziki Mnene lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania.Tamasha hilo lililoanza jijini Dar  es Salaam eneo la Boko mwishoni mwa wiki, litaendelea katika mkoani ya Pwani

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE, Bw. Edwin Rutageruka (kushoto) wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya bidhaa yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza , Bw. Lameck Borega (kushoto) ambaye ni Meneja wa Uwekezaji kutoka EPZA, Mabibo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia  Masuala ya Wakimbizi, Fillipo Grand kabla ya mazungumzo yao jijini Nairobi, Agosti  28, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa kitabu chenye picha ramani na taarifa za jiji la Yokohama nchini Japan na Meya wa jiji hilo, Bi. Fumiko Hayashi baada ya mazungumzo yao jijini Nairobi Agosti 28, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa maonyesho kutoka Senegal wakati alipotembelea bada lao kwenye  maonyesho yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitazama nguo za batik wakati alipotembelea banda la Tanzania kwenye   maonyesho yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais na Ofisa mtendaji Mkuu wa kampuni ya Sumitomo Corporation ya Japan, Bw. Kunihuru Nakamura  katika Mkutano wa TICAD 6 uliofanyika Nairobi Kenya, Agosti 28, 2016

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais na Ofisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sumimoto Corporation ya Japan katika mkutano wa TICAD 6 uliofanyika jijini Nairobi
i

No comments :

Post a Comment