Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na Balozi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shio (katikati) kulia ni Waziri
Mambo ya Njena ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano
wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC Troika
Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini
mwa Afrika umefanyika mchana huu katika
ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
Hii
ndio muonekano wa Ukumbi wa Mkutano wa Mandvulo Grand uliopo Lozitha
mjini Mbabane Swaziland ambapo mkutano wa 36 SADC unafanyika.
Mkutano wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika
Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika umefanyika mchana huu katika
ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
Mkutano huo
wa Troika unaohusisha nchi Tatu ambazo ni za Utatu ikiwemo Tanzania, Msumbiji
na Afrika Kusini ambapo kwa kuzingatia utaratibu huo mkutano huo unahudhuriwa
na Wakuu wa nchi na serikali wa Msumbiji kama Mwenyekiti wa Asasi hiyo (SADC
Organ Troika Summit) na Afrika Kusini kama mwenyekiti aliyetoka na Tanzania
inatarajiwa kukabidhi uenyekiti wa Asasi hiyo.
Baadhi ya
ajenda ambazo viongozi hao watajadili kwenye mkutano huo ni hali ya ulinzi na
usalama katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Lesotho,
masuala ya upatanishi na utatuzi wa migogoro pamoja na maombi ya Burundi na
Comoro kutaka kujiunga katika Jumuiya ya Mandeleo Kusini mwa Afrika- SADC.
Katika
mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Ufunguzi
rasmi wa mkutano wa SADC utafanyika terehe 30-Aug-16 katika ukumbi wa Grand-
Lozitha mjini Mbababe Swaziland ambapo pamoja na Mambo mengine mkutano huo
utatoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda katika uandishi wa insha katika jumuiya
hiyo.
MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA JWTZ, JKT MGULANI YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM
Meja Dora Kawawa wa Kikosi cha Jeshi la
Kujenga Taifa 831 KJ Mgulani (kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula,
Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini,
Beatrice Lawrance, Dar es Salaam leo jioni , ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ), ambapo kilele chake kitakuwa Septemba Mosi mwaka huu.
Maofisa wa Jeshi wa kikosi hicho wakifurahi na watoto wa kituo hicho baada ya kutoa msaada wao.
Msaada ukitolewa.
Hapa ni furaha pamoja na watoto hao.
Watoto wakipata msaada huo.
Watoto wakipokea msaada.
Hapa ni furaha tupu kwa watoto kwa kupokea msaada kutoka kwa wazazi wao hao.
Picha ya pamoja na watoto hao na viongozi wao.
Na Dotto Mwaibale
JESHI la Kujenga Taifa Kikosi 831 Kj
Mgulani limetoa msaada wa vyakula na sabuni kwa watoto waishio Makao ya
Taifa ya Watoto Wenye Shida Kurasini jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada
huo kwa niaba ya mkuu wa kikosi hicho Dar es Salam , Meja Dora Kawawa
alisema ni moja ya sehemu ya maadhimisho ya kusherehekea miaka 52 tangu
kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
"Tumeamua kushiriki shughuli za kijamii
kama kutoa msaada na kufanya usafi ikiwa ni kuadhimisha siku ya
kuanzishwa kwa jeshi letu ambapo kilele chake kitakuwa Septemba mosi
mwaka huu" alisema Kawawa.
Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya
Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance alishuru JKT kwa msaada
huo na kueleza ni muhimu sana kwa watoto hao na kuomba taasisi nyingine
kuiga mfano huo ili kujenga taifa bora la kesho.
Wananchi wakiangalia ajali
iliyosababishwa na daladala lenye namba za usajili T 397 BVB linalofanya
safari zake kati ya Temeke na Gongo la Mboto kwa kuyagonga magari
mengine matatu eneo la Maji Matitu Temeke Dar es Salaam leo asubuhi.
Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo namba T 628 DFE alijeruhiwa.
Gari dogo namba T 628 DFE lililogongwa na daladala hilo likiwa limeharibika.
Daladala hiloegonga gari namba T 458 CAN.
Kuku waliokuwa kwenye moja ya gari lililogongwa wakiondolewa kuku kadhaa walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Askari wa Usalama barabarani akiangalia ajali hiyo.
Daladala uso kwa uso na gari dogo.
Na Dotto Mwaibale
MKAZI wa Chamazi ambaye ni mwanamke
amejeruhiwa baada ya gari lake dogo alilokuwa akiendesha kugongwa na
daladala lenye namba T 397 BVB linadodaiwa kuiba njia.
Ajali hiyo imetokea Maji Matitu Temeke
jijini Dar es Salaam leo asubuhi ambapo daladala hilo pia liliyagonga
magari mengine matatu na kuzua kizaazaa katika barabara ya Charambe
kwenda Chamazi.
Mkazi wa eneo hilo Hamisi Juma
aliyeshuhudia ajali hiyo amesema ni mungu kasaidia kutokea kwa vifo
kwani ajali hiyo ilikuwa ni mbaya sana.
" Saa 12 na dakika 55 nikiwa nasubiri
gari kwenda kazini niliona daladala lililokuwa likitoka Charambe kwenda
Chamazi lilikuwa likipita upande ambao si wake likiwa katika mwendo wa
kasi na ghafla lililigonga gari dogo namba T 628 DFE ambalo ligeuka na
kulala katika mtaro" alisema Juma.
Alisema baada ya kuligonga gari hilo
liliyaparamia magari mengine madogo mawili likiwepo lililobeba kuku na
kuyasukumia kwenye mtaro.
Aliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo dereva wa daladala hilo alikimbia na kulitelekeza gari lake.
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T 628 DFE, T 397 BVB, T 451 CQB na T 458 CAN.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Temeke ili kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda baada ya
simu yake kuita bila kupokewa alipopigiwa simu mara kadhaa.
Msanii Joh Makini akiwarusha mashabiki wa hip hop kwenye Tamasha la Tigo Fiesta wilaya Muleba usiku wa jana lililofanyika uwanja wa David Zihimbile. |
Meya wa Manispaa ya Kinondoni jijini
Dar es Salaam, Boniface Jacob, (watatu kushoto), na Mbunge wa Kawe,
Halima Mdee (wanne kushoto), wakiongozana na wananchi na baadhi
yaviongozxi wa wilaya hiyo, wakati wa ziara ya kutembelea eneo la
mgogoro huko Kunduchi Mecco Mji mpya jijini Dar es Salaam.
BARAZA Kuu la Uongozi la Chama Cha
Wananchi CUF, lililoketi mjini Unguja Jumapili Agosti 28, 2016, limewasimamisha
uanachama aliyekuwa Mswenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Magdalena Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa
Kaliua mkoani Tabora.
Katika taarifa yake kwa v yombo vya
habari iliyotolewa leo Agosti 29, 2016 makao makuu ya chama hicho Vuga kisiwani
Unguja, Viongozi hao pia watatakiwa kujieleza mbele ya baraza hilo kwa hatua
zaidi.
Taarifa ya Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar),
Nassor Ahmed Mazrui, alisema uamuzi wa kuwasimamisha uanachama viongozi hao
umezingatia Katiba ya Chama, Ibara ya 83 (5)(c), hadi hapo watakapopata fursa
ya kujieleza mbele ya Baraza Kuu
Pia Baraza hilo limetoa karipio kali kwa
viongozi kadhaa, chini ya Ibara ya 83
(5)(b) ambao ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa 1. Rukiya Kassim
Ahmed na
2. Athumani Henku
Viongozi wengine waliosimamishwa
uanachamasambamba na Profesa Lipumba na Sakaya ni pamoja na
3. Abdul Kambaya
4. Ashura Mustafa
5. Omar Mhina Masoud
6. Thomas Malima
7. Kapasha M. Kapasha
8. Maftaha Nachumu
9.Mohamed Habib Mnyaa
10. Haroub Shamis
na
na
11. Mussa Haji Kombo
Mwanachama aliyefukuzwa chama ambaye
alipata fursa ya kujieleza mbele ya Baraza Kuu na kikao kuamua kumfukuza chama
kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 83 (5)(c) ni aliyekuwa Kaimu Katibu
Mtendaji wa Jumuiya ya Wazee wa CUF (JUWACUF), Shashu Lugeye.
Kufuatia maamuzi hayo, Baraza Kuu la
Uongozi la Taifa limewateua viongozi mbali mbali kukaimu nafasi mbali mbali
zilizoachwa wazi.
Kwa kuzingatia kwamba kutokamilika kwa
Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa tarehe 21 Agosti, 2016 kulipelekea kushindwa
kufanyika kwa uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama, Baraza Kuu
la Uongozi la Taifa limetumia uwezo liliopewa na Katiba ya Chama, Ibara ya 101
na 118, kuunda Kamati ya Uongozi ambayo itakuwa ikifanya kazi za Mwenyekiti na
Makamu Mwenyekiti hadi hapo uchaguzi wa kujaza nafasi hizo utakapofanyika.
Baraza Kuu la Uongozi limewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati hiyo ya
Uongozi:
1. Mhe. Julius Mtatiro – Mwenyekiti;
2. Mhe. Katani Ahmed Katani – Mjumbe; na
3. Mhe. Severina Mwijage – Mjumbe.
Aidha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa,
kwa kufuata Ibara ya 105 (1) na (3) ya Katiba ya Chama, limemteua Mhe. Joran
Bashange kuwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Chama kwa upande wa Tanzania Bara na
Mhe. Mbarala Maharagande kuwa Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na
Mawasiliano kwa Umma hadi hapo nafasi hizo zitakapojazwa rasmi kwa mujibu wa
masharti ya Katiba ya Chama.
Mwisho, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa
linawahakikishia wanachama na wapenzi wake na Watanzania wote kwa ujumla kuwa
Chama Cha Wananchi – CUF kipo imara na makini na katu hakitoyumbishwa kwa hila
na njama ovu na chafu zinazofanywa na maadui wa chama hichi. Tangu kuasisiwa
kwake, CUF imeandamwa na maadui wa kila aina, na imepitia katika misuko suko
mingi. Tunaamini hila na njama hizo ovu zimekuwa zikielekezwa CUF kwa kutambua
kwamba Chama hichi ndicho kinachobeba dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko ya
kweli hapa nchini.
Kutokana na umadhubuti, umakini na
uimara wa Katiba ya Chama na safu ya viongozi wake, CUF imeweza kuvuka salama
kila ilipoingia katika misuko suko hiyo na kwa hivyo, hata wimbi hili
lililoonekana kukitikisa Chama limekabiliwa ipasavyo na sasa kazi iliyopo mbele
yetu ni kuendeleza harakati za kisiasa za kuwaletea Watanzania wa Bara na
Zanzibar mabadiliko wanayoyataka.
Mgeni Rasmi Bibi.
Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (aliyesimama) akitoa
hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma kwa Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango
kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi. Wengine ni Bi. Lorah
Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango
(kushoto) na Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya
Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi
Jumla, Tume ya Mipango, Lorah Madete, akitoa neno kwa Maofisa na watendaji wa
Idara za Sera na Mipango kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi
ambao ni washiriki wa mafunzo yanayohusu Mwongozo
wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili afungue
mafunzo hayo ya siku tano. Waliokaa ni
Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (katikati) na Dr.
Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam
Washiriki wa
Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma ambao ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango
kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi wakimsikiliza kwa makini
Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika
Mkoani Tabora.
Washiriki wa
Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma ambao ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango
kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga na Katavi wakimsikiliza kwa makini
Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika
Mkoani Tabora.
Picha ya pamoja
(PICHA
ZOTE NA: THOMAS NYINDO-TUME YA MIPANGO)
i
Wakazi wa Boko jijini Dar es Salaam wakihangaika kucheza muziki wa
Singeli kwenye tamasha la Muziki Mnene lililodhaminiwa na Vodacom
Tanzania.Tamasha hilo lililoanza jijini Dar es Salaam eneo la Boko
mwishoni mwa wiki, litaendelea katika mkoani ya Pwani
Msaanii wa Muziki wa Singeli, Machupa akikonga mioyo ya wapenzi wa
muziki huo kwenye tamasha la Muziki Mnene lililodhaminiwa na Vodacom
Tanzania.Tamasha hilo lililoanza jijini Dar es Salaam eneo la Boko
mwishoni mwa wiki, litaendelea katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.
Wakazi wa Boko jijini Dar es Salaam wakihangaika kucheza muziki wa
Singeli kwenye tamasha la Muziki Mnene lililodhaminiwa na Vodacom
Tanzania.Tamasha hilo lililoanza jijini Dar es Salaam eneo la Boko
mwishoni mwa wiki, litaendelea katika mkoani ya Pwani
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu
Mkurugenzi wa TANTRADE, Bw. Edwin Rutageruka (kushoto) wakati alipotembelea
banda la Tanzania katika maonyesho ya bidhaa yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6
jijini Nairobi Agosti 28, 2016. (PICHA
NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza , Bw. Lameck Borega
(kushoto) ambaye ni Meneja wa Uwekezaji kutoka EPZA, Mabibo jijini Dar es
salaam wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho yaliyokwenda
sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Mataifa
anayeshughulikia Masuala ya Wakimbizi, Fillipo Grand kabla ya mazungumzo
yao jijini Nairobi, Agosti 28, 2016
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akikabidhiwa kitabu chenye picha ramani na taarifa za jiji la Yokohama
nchini Japan na Meya wa jiji hilo, Bi. Fumiko Hayashi baada ya mazungumzo yao
jijini Nairobi Agosti 28, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa maonyesho
kutoka Senegal wakati alipotembelea bada lao kwenye maonyesho
yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nguo za batik wakati
alipotembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho yaliyokwenda sambamba
na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais na
Ofisa mtendaji Mkuu wa kampuni ya Sumitomo Corporation ya Japan, Bw. Kunihuru
Nakamura katika Mkutano wa TICAD 6 uliofanyika Nairobi Kenya, Agosti 28,
2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais na Ofisa mtendaji Mkuu
wa Kampuni ya Sumimoto Corporation ya Japan katika mkutano wa TICAD 6
uliofanyika jijini Nairobi
No comments:
Post a Comment