Na Christian Gaya-HakiPensheni Institute
Benki Kuu ya Tanzania imesema inaendelea kushiriki kikamilifu katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni, kwa kuuza dola ya Marekani kwa benki za biashara ikiwa ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kupunguza uhaba wa fedha za kigeni nchini
.Imesema ya kuwa mpango huu unalenga kuhakikisha kuna ukwasi
wa kutosha wa fedha za kigeni katika soko. Vilevile, mpango huu unalenga
kuhakikisha kuwa wananchi wenye uhitaji halali wa ya fedha za kigeni wanapata
huduma hiyo kwa bei ya soko kupitia Taasisi rasmi za fedha nchini.
Imesisitiza ya kuwa ni muhimu kwa wadau wote kuelewa kuwa
ushiriki wa Benki Kuu ya Tanzania katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni
unazingatia Sera ya Ushiriki katika Soko la Fedha za Kigeni (Foreign Exchange
Intervention Policy) yenye lengo la kukuza utulivu wa soko na kukidhi mahitaji
halali ya fedha za kigeni nchini.
No comments :
Post a Comment