Pages

Saturday, March 23, 2024

“Juhudi za kukabiliana na upungufu wa fedha za kigeni kuendelea”-Benki Kuu

Na Christian Gaya-HakiPensheni Institute 

Benki Kuu ya Tanzania imesema inaendelea kushiriki kikamilifu katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni, kwa kuuza dola ya Marekani kwa benki za biashara ikiwa ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kupunguza uhaba wa fedha za kigeni nchini

.

Imesema ya kuwa mpango huu unalenga kuhakikisha kuna ukwasi wa kutosha wa fedha za kigeni katika soko. Vilevile, mpango huu unalenga kuhakikisha kuwa wananchi wenye uhitaji halali wa ya fedha za kigeni wanapata huduma hiyo kwa bei ya soko kupitia Taasisi rasmi za fedha nchini.

Imesisitiza ya kuwa ni muhimu kwa wadau wote kuelewa kuwa ushiriki wa Benki Kuu ya Tanzania katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni unazingatia Sera ya Ushiriki katika Soko la Fedha za Kigeni (Foreign Exchange Intervention Policy) yenye lengo la kukuza utulivu wa soko na kukidhi mahitaji halali ya fedha za kigeni nchini.

No comments:

Post a Comment