Thursday, December 31, 2020

WASHINDI KAMPENI YA CHANJA KIJANJA NA EXIM MASTERCARD WAENDELEA KUJINYAKULIA ZAWADI


 
Afisa Mwandamizi Huduma kwa wateja benki ya Exim Bi Farida Chambo  (kulia) akikabidhi zawadi ya simu kwa mmoja wa washindi wa wiki wa kampeni ya  'Chanja Kijanja na Exim  MasterCard' ya benki hiyo Bw Krushant Buhecha wa jijini Dar es Salaam. Pamoja na zawadi nyingine washindi wa kampeni hiyo watajipatia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu za ada ya shule kwa mtoto pamoja na vifaa vyote vya shule sambamba na safari za kwenda Serengeti na  Zanzibar wakiwa na wenza wao huku kila kitu kikiwa kimelipiwa.
Meneja Mwandamizi wa benki ya Exim Zanzibar Bw Mwinyimkuu Ngalima (kulia) akikabidhi zawadi ya simu kwa mmoja wa washindi wa wiki wa kampeni ya  'Chanja Kijanja na Exim  MasterCard' ya benki hiyo Bi Amani Makungu wa Zanzibar. Pamoja na zawadi nyingine washindi wa kampeni hiyo watajipatia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu za ada ya shule kwa mtoto pamoja na vifaa vyote vya shule sambamba na safari za kwenda Serengeti na  Zanzibar wakiwa na wenza wao huku kila kitu kikiwa kimelipiwa.

 

No comments :

Post a Comment