Friday, July 31, 2020

DK SHEIN AAGA RASMI ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akizungumza katika Baraza la Eid, lililofanyika Bumbwini, Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Dkt. Shein ametumia sherehe hizo kuaga rasmi wananchi wa Zanzibar. Picha zote kwa hisani ya Mwinyi2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, ametumia Baraza la Eid, lililofanyika Bumbwini, Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja kuaga rasmi wananchi wa Zanzibar. Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali. Sherehe hizo zilitanguliwa na Swala ya Eid iliyoswaliwa katika viwanja vya Misuka, Mahonda.
 
Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgombea Urais Mteule wa Chama Cha Mapinduzi, CCM Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika sherehe hizo zilizotanguliwa na Swala ya Eid iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Misuka, Mahonda.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na kuzungumza na  Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwenye sherehe hizo zilitanguliwa na Swala ya Eid.
 
Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi na wwageni waalikwa kwenye sherehe hizo zilitanguliwa na Swala ya Eid iliyoswaliwa katika viwanja vya Misuka, Mahonda. Picha kwa hisani ya Mwinyi2020.
 

 
Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na viongozi wengine wakishiriki Swala ya Eid iliyoswaliwa katika viwanja vya Misuka, Mahondawa.
 
Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali wakiwa katika sherehe hizo.
 
 
Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali wakiwa katika sherehe hizo.
 
Swala ya Eid iliyoswaliwa katika viwanja vya Misuka, Mahonda ikiendelea. Picha kwa hisani ya Mwinyi2020.

Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akisalimiana na viongozi mbalimbali na wageni waalikwa katika sherehe hizo.
 
Mgombea Urais Mteule wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akisalimiana na viongozi mbalimbali na wageni waalikwa katika sherehe hizo. Picha zote kwa hisani ya Mwinyi2020.

No comments :

Post a Comment