**********************************
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais
TAMISEMI Selemani Jafo amefurahishwa na utendaji kazi wa Viongozi na
watendaji wa Mkoa na Jiji la Mbeya kwa kusimamia kazi bila kufanya
maigizo.
Jafo aliyasema hayo wakati wa Ziara ya kikazi aliyoifanya Mkoani humo leo hii akikagua
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katika ziara hiyo Waziri Jafo
alikagua na kuweka jiwe la msingi ya shule mpya ya Msingi iitwayo
Magufuli inayojengwa katika jiji la Mbeya, ujenzi wa Ofisi mpya ya Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, pamoja na ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya
Mbeya.
Mkoa wa Mbeya umepokea shilingi
bilion 2.1 kwaajili ya kuanza ujenzi wa Ofisi ya Mkoa, shilingi milion
790 kwaajili ya ukarabati wa shule kongwe ya Mbeya ambapo kazi hizo zote
zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Akiongea na wanafunzi wa kidato
cha sita wa sekondari ya Mbeya waliorejea shuleni hapo leo hii kwa
maelekezo ya Serikali, Waziri Jafo amewataka wanafunzi hao kuendelea
kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo yote yaliyo tolewa na serikali
juu ya kujilinda na janga la korona huku wakijiandaa na maandalizi ya
mitihani yao itakayoanza ndani ya mwezi huu wa Juni
No comments :
Post a Comment