29/04/2020 JIJINI DODOMA
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas ameeleza Jeshi la Polisi nchini linaendelea kufanya Operesheni ya kuwakamata wafanyabiashara wanaouza sukari kinyume na bei elekezi ya serikali, Operesheni hiyo ambayo ilianza kufanyika 25/04/2020 ikiongozwa na
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Bodi ya Sukari, Tume ya Ushindani pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania ambapo hadi sasa imefanikiwa kuwakamata Jumla ya watuhumiwa 36 katika mikoa ya Dar Es Salaam,
Morogoro, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro na Tanga huku jumla ya tani 106,939 za sukari zikiwa zimekamatwa katika mikoa hiyo.
Aidha, Kamishna Sabas amesema kuwa, hali ya nchi yetu kwa sasa ni shwari hakuna matishio yoyote ya kiuhalifu na kwamba operesheni mbalimbali ikiwemo misako bado zinaendelea huku akiwataka wananchi kutokuogopa vipima joto vinavyotumiwa na Jeshi la Polisi wawapo vituoni kwa ajili ya kukabiliana na janga la Virusi Corona.
No comments :
Post a Comment