Idadi
ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani imeongezeka na
kufikia zaidi ya Milioni moja, huku idadi ya watu walipoteza maisha
ikifikia zaidi ya... 58,000.
Takwimu
za kiafya zinaonesha kuwa kwa sasa Marekani ina visa vya maambukizi
1,035,765 huku idadi ya watu walipoteza maisha ikifikia zaidi ya Elfu
59.
Wachambuzi
wa mambo nchini humo wanasema idadi ya watu walipoteza maisha sasa
inazidi ile iliyoshuhudiwa wakati wa vita nchini Vietnam.
Kulingana
na ripoti ya Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, watu 59,266 wamefariki dunia
kwa ugonjwa wa Covid-19 nchini Marekani, nchi iliyoathirika zaidi
ulimwenguni, wakati askari 58,220 wa nchi hiyo walipoteza maisha wakati
wa vita vya Vietnam (1955-1975), kulingana na ripoti rasmi
iliyochapishwa kwenye Jalada la kitaifa.
Ongezeko
la maambukizi na vifo linatishia hatma ya kisiasa ya rais Donald Trump
ambaye atatetea kiti chake wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.
No comments :
Post a Comment