Pages

Wednesday, April 29, 2020

Idadi ya Vifo Vya Corona Nchini Marekani Yazidi Idadi ya Wamarekani Waliofariki Wakati wa Vita Vya Vietnam


Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani imeongezeka na kufikia zaidi ya Milioni moja, huku idadi ya watu walipoteza maisha ikifikia zaidi ya... 58,000.

Takwimu za kiafya zinaonesha kuwa kwa sasa Marekani ina visa vya maambukizi 1,035,765  huku idadi ya watu walipoteza maisha ikifikia zaidi ya Elfu 59.

Wachambuzi wa mambo nchini humo wanasema idadi ya watu walipoteza maisha sasa inazidi ile iliyoshuhudiwa wakati wa vita nchini Vietnam.

Kulingana na ripoti ya Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, watu 59,266 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 nchini Marekani, nchi iliyoathirika zaidi ulimwenguni, wakati askari 58,220 wa nchi hiyo walipoteza maisha wakati wa vita vya Vietnam (1955-1975), kulingana na ripoti rasmi iliyochapishwa kwenye Jalada la kitaifa.

Ongezeko la maambukizi na vifo linatishia hatma ya kisiasa ya rais Donald Trump ambaye atatetea kiti chake wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.

No comments:

Post a Comment