Wednesday, March 4, 2020

ZOEZI LA KUSAJILI WATOA HUDUMA WA FEDHA KUANZA MWEZI HUU-BOT


Mkuurgenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Bernard Dadi akiwasilisha mada kuhusu Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma wa kifedha_(Financial Service Register) katika semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha jijini Arusha, Machi 4, 2020.
Meneja wa Idara ya Uhusioano wa Umma na Itifaki, Bi. Zalia Mbeo, (kulia), akizungumza kuhusu namna mafunzo hayo yalkivyoendeshwa.






NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
USAJILI wa watoa huduma wa Fedha unaanza mwezi huu wa Machi, 2020 Mkuurgenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Bernard Dadi amesema.
Bw. Dadi amesema zoezi hilo litafanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza (first phase) itaanza Machi na kukamilika Aprili mwaka huu na  itahusisha mikoa iliyoko eneo la Kaskazini mwa nchi linalotengwa na reli ya Kati, huku awamu ya pili (second phase) itaanza mwezi Mei na kukamilika mwezi Juni ambapo mikoa itakayohusika ni le iliyo katika upande wa Kusini mwa reli ya Kati zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei hadi Juni, 2020.
Akiwasilisha mada kuhusu Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma wa kifedha_(Financial Service Register) katika semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha jijini Arusha, Machi 4, 2020.
“Kila mtoa huduma lazima ajisajili vinginevyo hawezi kuendelea kutoa huduma hiyo kwa vile mfumo hautamtambua.” Alisisitiza.
Akieleza sababu za kuanzishwa kwa mfumo huo Bw. Dadi alisema, kukidhi matakwa ya sheria ya Mifumo ya malipo ya Taifa (NPS Act ya 2015), upatikanaji wa taarifa zinazoendana na wakati na timilifu, upimaji wa viashiria vya Mpango Mkakati wa huduma jumuishi za kifedha (NFIF), kuwezesha maamuzi ya kibiashara na mipango mkakati na kusaidia utambuzi wa maeneo yenye ukosefu wa huduma.
Aidha usajili huo uko katika makundi manne, ambayo ni pamoja na mawakala wakuu (seper agents) hawa ndio wanasimamia flots na hawa super agents wako wachache ikiwa ni pamoja na matawi ya mabenki ya biashara, Watoa huduma kwenye maduka (KYC), ambao sheria inawataka wawe na duka na sehemu inayoeleweka, (tambulika), huku kundi la tatu ni wale  wenye viosky (M-pesa, tiGO-pesa, Airtel Money na Halopesa,na kundi la mwisho ni lile linalowahusu watoa huduma   wanaoendesha shughuli zao chini ya mawakala wakubwa (Super agents) na hawa ndio wengi wanapatikana kila mahali huko mitaani.
Alisema makundi hayo yote yatasajiliwa kulingana na vigezo vinavyowekwa na BoT ili kuhakikisha fedha za walaji zinakuwa salama.
“Ili mtu aweze kusajiliwa lazima awe na kitambulisho kimoja kati ya vitambulisho vitano vinavyotambuliwa na Benki Kuu ambavyo ni Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi, Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha kupigia kura au Pasi ya Kusafiria.” Alifafanua.
Hata hivyo alisema masharti ya usajili kwa kundi la mwisho ni yatazingatia utaratibu unaotumiwa kati ya Wakala mkubwa (Super agent) wa kampuni ya simu na wakala mdogo.
Alisema BoT imekasimu shughuli hizo za usajili kwenye Halmashauri mbalimbali kote nchini na kwamba mawakala wadogo wa kundi la nne ambao ndio wengi wasiwe na wasiwasi kwani huudma hizo zitatolewa kwenye ngazi ya serikali za Mitaa chini ya Taasisi ya Financial Sector Development Trust (FSDT). Alisema Bw. Dadi.

No comments :

Post a Comment