Mkuurgenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), Bw. Bernard Dadi akiwasilisha mada kuhusu Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma wa kifedha_(Financial Service Register) katika semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha jijini
Arusha, Machi 4, 2020.
Meneja wa Idara ya Uhusioano wa Umma na Itifaki, Bi. Zalia Mbeo, (kulia), akizungumza kuhusu namna mafunzo hayo yalkivyoendeshwa. |
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
USAJILI
wa watoa huduma wa Fedha unaanza mwezi huu wa Machi, 2020 Mkuurgenzi wa Mifumo
ya Malipo ya Taifa, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Bernard Dadi amesema.
Bw.
Dadi amesema zoezi hilo litafanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza (first phase) itaanza Machi na kukamilika
Aprili mwaka huu na itahusisha mikoa
iliyoko eneo la Kaskazini mwa nchi linalotengwa na reli ya Kati, huku awamu ya
pili (second phase) itaanza mwezi Mei
na kukamilika mwezi Juni ambapo mikoa itakayohusika ni le iliyo katika upande
wa Kusini mwa reli ya Kati zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei hadi Juni, 2020.
Akiwasilisha
mada kuhusu Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma wa kifedha_(Financial Service Register) katika
semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha jijini Arusha, Machi 4, 2020.
“Kila
mtoa huduma lazima ajisajili vinginevyo hawezi kuendelea kutoa huduma hiyo kwa
vile mfumo hautamtambua.” Alisisitiza.
Akieleza
sababu za kuanzishwa kwa mfumo huo Bw. Dadi alisema, kukidhi matakwa ya sheria
ya Mifumo ya malipo ya Taifa (NPS Act ya 2015), upatikanaji wa taarifa
zinazoendana na wakati na timilifu, upimaji wa viashiria vya Mpango Mkakati wa
huduma jumuishi za kifedha (NFIF), kuwezesha maamuzi ya kibiashara na mipango
mkakati na kusaidia utambuzi wa maeneo yenye ukosefu wa huduma.
Aidha
usajili huo uko katika makundi manne, ambayo ni pamoja na mawakala wakuu (seper
agents) hawa ndio wanasimamia flots na hawa super agents wako wachache ikiwa ni
pamoja na matawi ya mabenki ya biashara, Watoa huduma kwenye maduka (KYC), ambao
sheria inawataka wawe na duka na sehemu inayoeleweka, (tambulika), huku kundi
la tatu ni wale wenye viosky (M-pesa,
tiGO-pesa, Airtel Money na Halopesa,na kundi la mwisho ni lile linalowahusu
watoa huduma wanaoendesha shughuli zao chini ya mawakala
wakubwa (Super agents) na hawa ndio wengi wanapatikana kila mahali huko
mitaani.
Alisema
makundi hayo yote yatasajiliwa kulingana na vigezo vinavyowekwa na BoT ili
kuhakikisha fedha za walaji zinakuwa salama.
“Ili
mtu aweze kusajiliwa lazima awe na kitambulisho kimoja kati ya vitambulisho
vitano vinavyotambuliwa na Benki Kuu ambavyo ni Kitambulisho cha Taifa,
Kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi, Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha kupigia kura
au Pasi ya Kusafiria.” Alifafanua.
Hata
hivyo alisema masharti ya usajili kwa kundi la mwisho ni yatazingatia utaratibu
unaotumiwa kati ya Wakala mkubwa (Super
agent) wa kampuni ya simu na wakala mdogo.
Alisema
BoT imekasimu shughuli hizo za usajili kwenye Halmashauri mbalimbali kote
nchini na kwamba mawakala wadogo wa kundi la nne ambao ndio wengi wasiwe na
wasiwasi kwani huudma hizo zitatolewa kwenye ngazi ya serikali za Mitaa chini
ya Taasisi ya Financial Sector Development Trust (FSDT). Alisema Bw. Dadi.
No comments:
Post a Comment