Pages

Wednesday, March 4, 2020

Kamati ya Maridhiano Mkoa wa Morogoro waiongeza TCRA kwa kuwapa elimu ya Mawasiliano



Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Morogoro wakiwa katika Semina ya TCRA kuhusiana na utumiaji wa huduma za Mawasiliano ikiwa ni Kampeni Sirubuniki kuwa Mjanja.
Kaimu Katibu wa Mkoa wa Baraza la Miskiti Tanzania (Bamita) Abdul Koba akizngumza katika Semina ya Amani Mkoa wa Morogoro iliyotolewa na TCRA kuhusiana na utumiaji wa huduma za mawasiliano.
Juma Yahaya Ng’ondavi – Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Mkoa Morogoro akichangia Semina ya Kamati Amani Mkoa wa Morogoro iliyotolewa na TCRA.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akizungumza wakati wa Semina ya Kamati ya Amani ya Mkoa Morogoro kuhusiana utumiaji wa huduma za Mawasiliano ikiwa ni Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.
**************************
Kamati ya Amani mkoa wa Morogoro imesema kuwa elimu ya utumiaji wa huduma za
mawasiliano imefika kwa wakati mwafaka kutokana na teknolojia hiyo kukua kila siku.
Wameyasema hayo wakati wa Semina ya Kamati ya Amani ya Mkoa Morogoro inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoa elimu juu ya utumiaji wa huduma za mawasiliano kwa kujinga na Uhalifu unapotumia huduma hizo.
TCRA ipo katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja ambayo inakwenda katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani katika kutoa elimu hiyo utumiaji wa huduma za mawasiliano.
Akizungumza katika Semina hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano wa Kamati ya Amani Mkoa wa Morogoro Juma Ng’ondavi amesema kupata Semina ya huduma za mawasiliano kuna umuhimu kutokana na wao wanazunguka jamii yote ya Mkoa huo.
Amesema kuwa Kazi yao ni pamoja kuwa mabalozi kwa viongozi ambao hawajafika kuendelea kutoa elimu katika ibada ili waumini waweze kupokea elimu ya kujikinga na uhalifu wakati unapotumia huduma za mawasiliano.
Katibu wa Makanisa Mkoa wa Morogoro na Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Mkoa huo Mchungaji Canon Regnald Mdugi amesema elimu waliopata TCRA wataipeleka kwa waumini kwa kuhakikisha wanaelewa katika kujikinga na uhalifu wakati kutumia mitandao ya mawasiliano.
Amesema viongozi wa dini kazi yetu ni kuitumia elimu hii na kuipeleka kwa waumini kwa ustawi wa nchi yetu
Kampeni ya kuelimisha jinsi ya kujikinga na uhalifu wakati wa kutumia huduma za mawasiliano ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Sirubiniki Mjanja haingizwi chaka inayolenga katika kuelimisha umma ya kujikinga.
Wakichangia katika semina hiyo viongozi hao wamepongeza juhudi za Mamlaka ya Mawasiliano za kuwalinda wateja na kuahidi kushiriki katika kampeni hiyo.
Kamati hiyo imetoa wito kwa taasisi kuiga mfano wa TCRA katika kuelimisha viongozi wa dini wanawafuasi wengi na ushawishi mkubwa katika jamii.
Kampeni ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka imeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo cha uhalifu mitandaoni yenye lengo la kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga ili wasirubuniwe wanapotumia huduma za mawasiliano.
Kampeni ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania
Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo la kujenga maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali
Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Christopher John amesema kuwa viongozi wa dini ni watu mhimu sana katika kutoa elimu kwa waumini.
Amesema kuwa huduma za mawasiliano ni pana na teknolojia yake inabadilika kila siku
John amesema TCRA itaendelea kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya Mawasiliano kuhakikisha yanakuwa salama kwa ustawi wa nchi.
Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.
Amesema wakati amefikia wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi pamoja na wanaotumia mawasiliano bila kufuata sheria na taratibu mkono wa sheria utawakuta.

No comments:

Post a Comment