Mbunge wa Kawe, Mhe. Halima Mdee
akichangia jambo wakati wa Bunge la 11 Mkutano wa 19 kikao cha kwanza
kilichoanza leo Bungeni Jijini Dodoma huku Mkutano huo unatarajia
kumalizika tarehe 30 Juni, 2020.
………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mbunge wa jimbo
la Kawe jijini Dar Es Salaam Mhe.Halima Mdee ameishauri Serikali
kufanya mchakato wa kupima Corona wabunge wote na watakaobainika wawekwe
karantini.
Mhe.Mdee amesema
hayo leo bungeni jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa inatakiwa kila
mbunge apimwe homa ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona[COVID
-19]na akibainika na maambukizi ya virusi hivyo atengwe eneo
maalum[karantini] na wale watakaobainika kutokuwa na maambukizi
waendelee na mkutano ili kujadili bajeti kuu ya serikali ikiwa ni
mkutano wa Mwisho kuelekea uchaguzi mkuu.
“Leo
wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi wote,kwa nini tusipime wote
atakayebainika ana virusi apelekwe karantini na akiwa salama abaki hapa
kujadili mambo ya msingi kwa mstakabali wa taifa letu maana ni mkutano
wa mwisho”amesema Mdee
Naye,Mbunge wa
Iringa Mjini Mch.Peter Msigwa ameiomba serikali kuja na mpango wa
pamoja katika kujadili katika mapambano ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu
inayosababishwa na virusi vya corona[COVID-19].
Spika wa bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema katika
mkutano wa bunge la bajeti ni vyema majadiliano ya pande zote mbili
yakazingatiwa huku akitoa wito kwa wabunge kusikilizana na kuelekeza
zaidi kwenye bajeti kwani ni mkutano wa Mwisho ambapo bunge litavunjwa
kuelekea uchaguzi mkuu 2020.
“Kikao ni chetu
kisiwe cha upande mmoja au watu wachache hata kidogo kwa hiyo natoa wito
kusikilizana kwa pande zote mbili na ni vyema zaidi mbunge ukajielekeza
kwenye bajeti kuliko ukasimama na yako tu ni muhimu sana kuzingatia
muda”amesma.
Katika hatua
nyingine Mhe.Ndugai ametoa maelekezo kwa serikali kuandaa majibu haraka
iwezekanavyo juu ya Hoja Za Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Hesabu
za Serikali[CAG] zilizowasilishwa hivi karibuni kwa Mhe.Rais .
No comments :
Post a Comment