Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Nchini, Mh. Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akikata
utepe kuashiria Uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano wa TTCL katika kampeni
ya “SWITCH-ON, Mawasiliano kwa wote” katika kijiji cha Irkuishbo
wiliyani Kiteto mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Nchini, Mh. Atashasta Nditiye (wa pili kushoto)
akishangilia pamoja na wananchi wa kijiji cha Irkuishbor, Kiteto Mkoani
Manyara mara baada ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mnara
wa Mawasiliano wa TTCL.
…………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu,
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Nchini, Mh. Atashasta Nditiye Ijumaa ya
tarehe 28
Februari, 2020 amehitimisha Kampeni maalum ya Shirika la Mawasiliano
Nchini, TTCL ijulikanayo kama “SWITCH-ON, Mawasiliano kwa wote” kwa
mikoa ya Ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania katika kijiji cha Irkuishbor
wilayani Kiteto Mkoani Manyara.
Kampeni hiyo iliyoambatana na
zoezi la kuzindua Minara ya Mawasiliano ya Shirika hilo kwa ukanda wa
Kaskazini ilianzia Jijini Tanga tarehe 25 Februari, 2020 na kuendelea
katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na kuhitimishwa Mkoani Manyara.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri
aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano nchini, Bw.
Waziri Kindamba, Meneja Uhusiano wa Shirika hilo Bi. Puyo Nzalayaimisi
na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa ngazi za Mkoa wa Shirika hilo
kubwa la Mawasiliano.
Mh. Nditiye alisema Kampeni hii
itaendelea sehemu mbalimbali nchini ambazo zina changamoto ya
mawasiliano, “Nimeshiriki katika ziara hii ya kampeni ya SWITCN-ON,
Mawasiliano kwa wote, ambayo inasimamiwa na TTCL Corporation katika mkoa
wa Morogoro, Tanga, Kilimanjaro na Arusha. Nilizindua rasmi kampeni hii
katika kambi ya kikosi 121 Mkoani Morogoro Kidugala Sangasanga, baadaye
nikazindua Mnara wa Mawasiliano katika kata ya Masalai Muheza Tanga,
Kashashi Siha Kilimanjaro, Mundarara Longido Arusha na hatimaye
kuhitimisha katika wilaya hii ya Kiteto, Manyara na tutaendelea na zoezi
hili Nchi nzima kuweza kuwafikia wananchi wote”.
No comments :
Post a Comment