
Na.Ashura Mohamed -Arusha
Wataalamu wa Mionzi nchini
wametakiwa kuwa na weledi na kuongeza umakini katika
matumizi ya mionzi
salama ili kuhakikisha kuwa watanzania wanabaki salama.
Kufuatia Hali hiyo ambayo
inaelezwa kuwa sheria na taratibu zikifutwa hospitali nyingi hapa nchini
zitaepuka adha ya kufungiwa ikiwa zitakuwa na mashine zenye ubora
pamoja na watoaji wa huduma za mionzi waliobobea.
Kutokana na sheria kukiukwa jumla
ya hospitali 94 ambazo zinatoa huduma za Mionzi nchini zimefungiwa
kutokana na kutokidhi ubora wa utoaji huduma hiyo hapa nchini.
Akizungumza wakati wa kufunga
Mafunzo ya siku tano ya Uthibiti Usalama wa Mionzi katika idara ya
radiolojia nchini yaliyofanyika katika Kituo cha nguvu ya Atomik jijini
Arusha Mkurugenzi wa kituo hicho Profesa Lazaro Busagala alisema jumla
ya hospitali zilizofanyiwa Ukaguzi ni 664 ambapo hospitali 105
zilifungiwa kutokana na kutokukidhi vigezo vilivyopo.
Profesa alisema kuwa mara baada
ya ukaguzi Hospitali kumi tu zilifunguliwa kutokana na kukidhi vigezo na
kufunguliwa ambapo mpaka sasa 95 bado zimefunga kwa mujibu wa kaguzi za
mwaka 2019/2020.
Aidha aliwataka washiriki wa
Mafunzo hayo kuhakikisha kuwa wanatumia vyema taaluma zao katika
kuhakikisha kuwa watanzania haawaathiriki na Mionzi na pindi ambapo
wanaona kuna changamoto katika maeneo yao ya kazi basi waweze
kuhakikisha kuwa wanashauri kwa kutumia maandishi na sio maneno.
“Tutachukua hatua kali kwa wakuu
wa hospitali ambazo hazitafuata taratibu tutafungia moja baada ya
nyingine mpaka taratibu zitakapofuatwa ili watanzania waweze kuwa
salama”alisema profesa Busagala
Kwa Upande wake Mkurugenzi
Uthibiti na Usimamizi na Matumizi Salama ya Mionzi Dkt.Justine Ngaile
alisema kuwa baadhi ya mapungufu ambayo yanapelekea hospitali hizo
kufungwa ni pamoja na kukosa mtaalamu ambaye ana ubora wa kutoa huduma
hizo lakini pia Ubora wa mashine ambazo zinatumika kwenye huduma ya
mionzi kutokuwa na ubora ikiwa ni pamoja na Jengo linalohidhi mionzi
kutokuwa na ubora wa kutosha.
Hata hivyo dkt.Ngaile alisema
kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa mionzi hatarishi haiwezi kuwafikia
wataanzania na kuwaletea Athari bali wawe katika mikoni salama na
kuhakikisha kuwa wataalamu wanaongezewa ujuzi kutokana na mabadiliko ya
teknolojia.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa
teknolojia na Ufundi Filmi Banzi alisema kuwa Tanzania ipo salama kwa
kuwa tume ya nguvu za atomic ina ofisi zipatazo 26 mipakani kwa nchi
nzima ili kuzui vyanzo holela vya Mionzi ambavyo havihitajikikwa kutumia
vifaa maalum ambavyo ni gunduzi kwa mionzi isiyo salama.
Faustine Mulyutu ambaye ni katibu
wa wataalamu Mionzi Mikoa ya Tanzania Bara aliiomba serikali
kuhakikisha kuwa sekta ya wataalamu wa picha za mionzi inapewa
kipaumbele kama nyinginezo ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi
uliotukuka.
Jumla ya wataalamu wapatao 104
wamehudhuria mafunzo hayo wakiwa ni pamoja na mariadiojia,madaktari,na
wauguzi ambao wanahusikaa na namna moja ama nyingine na mionzi ya
mahospitalini.
No comments :
Post a Comment